VIONGOZI WA CCM WAASWA KUCHAGUA VIONGOZI MAKINI NA IMARA.
Balozi
Seif akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Tawi la Makangira Ndugu Haroub
Othman Mberwa aliyeuongoza ujumbe wa Viongozi kumi wa Kata hiyo
waliofanya ziara ya ujirani mwema hapa Zanzibar.
Mjumbe
wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Ujumbe
Viongozi wa CCM Tawi la Makangira Kata ya Msasani, Wilaya ya Kinondoni
Mjini Dar es salaam katika Banadari ya Malindi baada ya kumaliza ziara
yao ya ujirani mwema Visiwani Zanzibar wakiwa wenyeji wa Tawi la CCM
Vikokotoni Mjini Zanzibar.
Shirika la ndege la Etihad latoa taarifa kuhusiana na msukosuko wa Ndege yake Indonesia.
Vile vile walikutana na wanafamilia kadhaa wa majeruhi na
kuthibitisha kuwa shirika la ndege la Etihad litagharamia gharama zote
za matibabu.
Kati ya majeruhi tisa ambao walikuwa wamelazwa, wengi wao
wataruhusiwa kuondoka leo. Rais wa shirika la ndege la Etihad na
Mkurugenzi Mkuu Bwana James Hogan amesema: “Rubani wetu na wafanyakazi
wa ndege wanapaswa kupongezwa sana kwa utulivu wao na namna ambavyo
walishughulikia tukio hili la aina yake kwa utaalamu mkubwa, na huduma
waliyoionesha kwa abiria japo kuwa wengi wao walikuwa wamejeruhiwa. Ni
ushahidi wa mafunzo ya kiwango cha juu yanayotolewa kwa wafanyakazi wetu
ndio sababu athari za msukosuko ulipunguzwa. Wakati huo hakuna kabisa
usalama wa ndege,abiria au wafanyakazi walioathirika.”
Shirika la ndege la Etihad linashirikiana kikamilifu na Mamlaka za Indonesia katika uchunguzi wao.
MAJALIWA AKUTANA NA WAWEKEZAJI WA UMEME WA GESI TOKA JAPAN
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya KOYO ya
Japan, Bw. Norio Shoji baada ya kukutana na Mtendaji huyo na ujumbe
wake ofisini kwake jijini Dar es salaam May 9, 2016. Kampuni hiyo
ikishirikiana na Kampuni ya Kitanzania ya SSF Limited inakusudia
kuwekeza kwenye miundombinu ya umeme wa gesi asilia na jua nchini.
(Picha na ofisi ya Waziri Mkuu) .
No comments:
Post a Comment