N.I.H.F -KIKOA
N.I.H.F -KIKOA
FOREPLAN CLINIC
FOREPLAN CLINIC
Sunday, May 15, 2016
RAIS MSTAAFU AWAMU YA NNE DKT JAKAYA KIKWETE AMUWAKILISHA RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI MAZISHI YA LUCY KIBAKI NCHINI KENYA
Sunday, May 08, 2016
Maoni: 0
Mwili wa mke wa aliyekuwa rais wa Kenya Mwai kibaki , mama Lucy Kibaki ukiwasili kwa ajili ya maziko hapo jana katika eneo la Bunge la Odhaya kaunti ya Njeri,mjini Nairobi nchini Kenya.
Rais Mstaafu wa Tanzania Dkt Jakaya Kikwete akisalimiana na Rais Mstaafu wa Kenya Mh.Mwai Kibaki kufuatia kufiwa na mke wake mpendwa Mama Lucy Kibaki mjini Nairobi,nchini Kenya anaeshuhudia kulia ni Rais wa Kenya,Uhuru Kenyatta.
Naibu Rais wa Kenya Mh.William Rutto na Mkewe wakimfariji Rais Mstaafu wa Kenya Mh.Mwai Kibaki wakati wa mazishi ya Mkewe Lucy Kibaki yaliyofanyika jana katika eneo la Bunge la Odhaya kaunti ya Njeri,mjini Nairobi nchini Kenya,Pichani shoto ni Rais Mstaafu awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Kikwete akishuhudia tukio hilo.
Rais wa Kenya Mh Uhuru Kenyatta akizungumza jambo na Rais Mstaafu wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Jakaya Kikwete wakati wa mazishi ya Mama Lucy Kibaki hapo jana mjini Nairobi,kulia ni mke wa Rais Uhuru Kenyatta,Bi Margaret Kenyatta.
Rais Mstaafu wa Kenya,Mh.Mwai Kibaki akiweka udogo kwenye kaburi la Mke wake Mama Lucy Kibaki,wakati wa mazishi yaliyofanyika hapo jana katika eneo la Bunge la Odhaya kaunti ya Njeri,mjini Nairobi nchini Kenya.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta pamoja na Mkewe Margaret Kenyatta wakiweka udogo kwenye kaburi la mke wa aliyekuwa rais wa Kenya Mwai kibaki , mama Lucy Kibaki .Mazishi hayo yamefanyika jana katika eneo la Bunge la Odhaya kaunti ya Njeri,mjini Nairobi nchini Kenya.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta pamoja na Mkewe Margaret Kenyatta wakiweka shada la maua kwenye kaburi la mke wa aliyekuwa rais wa Kenya Mwai kibaki , mama Lucy Kibaki .Mazishi hayo yamefanyika jana katika eneo la Bunge la Odhaya kaunti ya Njeri,mjini Nairobi nchini Kenya,ambapo nchini Tanzania iliwakilishwa na Rais Mstaafu wa awamu ya nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Jakaya Kikwete kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.
Rais Mstaafu wa Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania Jakaya Kikwete amekuwa miongoni mwa viongozi wa ngazi za juu katika ukanda wa Jumuia ya Afrika Mashariki kuhudhuria hafla ya mazishi ya aliyekuwa mama wa Taifa la Kenya Bi Lucy Kibaki aliyefariki akiwa na miaka 82.
Marehemu Lucy Kibaki ametajwa na wanaomjua kama kiongozi aliyetetea mazingira safi ya kifamilia na alikuwa tayari kufanya kila jambo kuhifadhi utu na wema katika familia.
Kikwete ambaye aliwasilisha ujumbe wa Rais John Pombe Magufuli alisema kifo cha mama Lucy kibaki kimetokea wakati mchango wake ukiwa bado unahitajika katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na Naibu wake William Ruto waliohudhuria mazishi ya Bi Kibaki eneo la Bunge la Odhaya kaunti ya Njeri wamemtaja marehemu kama kiongozi aliyekuwa tayari kuhudumia taifa la Kenya.
RAIS DKT MAGUFULI ATANGAZA KUANZA KUKAMATWA KWA WAFICHA SUKARI NCHINI
Sunday, May 08, 2016
Maoni: 0
WAKAZI WAWILI MKOA WA KAGERA WAIBUKA WASHINDI PROMOSHENI YA SHINDANO LA PATA PATIA YA NMB BENKI
Sunday, May 08, 2016
Maoni: 0
Na Editha Karlo blog ya Jamii, Kagera.
WAKAZI wawili wa Mkoa wa Kagera wameshinda fedha taslimu kupitia shindano la pata patia linaloendeshwa na bank ya NMB katika matawi yake yote nchini.
Wakiongea na mtandao huu mara baada ya kushinda fedha hizo mmoja wa washindi hao Jafram Mohamed ambaye ni askari polisi Wilayani Ngara alisema kuwa anaupongeza uongozi wa NMB kwa kuanzisha shindano hilo kwa wateja wao kwani lina lenga kuwahamasisha kujiwekea akiba mara kwa mara.
Mohamed alisema kuwa yeye ni mtumishi wa serekali lakini amekuwa akijiwekea akiba mara nyingi kadiri awezavyo katika akaunti yake hali iliyopelekea kuingia katika droo ya kucheza bahati nasibu hiyo.
"Nilifurahi sana baada ya meneja kunipigia simu na kuniambia nimeingia faini za bahati nasibu ya shindano la pata patia, hizi fedha nilizoshinda shilingi laki nane ntazifanyia jambo la msingi na ambalo ni kumbukumbu kwangu na familia yangu"alisema Mohamed.Naye mshindi mwingine Philbert Robart mjasiliamali na mkazi wa Wilaya ya Muleba alisema kuwa amefarijika kushinda kiasi cha shilingi laki nne katika bahati nasibu ya pata patia toka bank ya NMB.
"Kwakweli bank ya NMB unatujali sana wateja wake, hizi fedha nilizoshinda leo zitanisaidia katila biashara zangu, nina wasihi wateja wote wa bank ya NMB nchi nzima wale wapya na wazamani kujiwekea fedha mara kwa mara katika akaunti yao itawapa nafasi ya kuingia katika shindano hili"alisema Rogati
Meneja wa NMB Mkoa wa Kagera Victorine Kimario alisema kuwa shindano hilo la pata patia kwa wateja wao ni endelevu hivo amewataka wateja kujiwekea fedha kwenye akaunti zao mara kwa mara ili waweze kupata nafasi ya kuingia kwenye droo ya kushinda.
''Kampeni hii ya pata patia ya kuwataka wateja wetu kuweka fedha katika akaunti zao imeanza mwezi wa pili mwaka huu, wateja wanatakiwa kuweka fedha katika akaunti zao kuanzia kiasi cha shilingi elf hamsini na kuendelea mara kwa mara ili aweze kuingia katika faini za kushinda"alisema Meneja
Alisema kila mteja ambaye anaingia fainali lazima ashinde sababu atatakiwa kuzungusha gurudumu lenye lenye nba kuanzia laki moja hadi milioni tatu na mshale wa gurudumu utakaposimama ndiyo kiasi ambacho atakuwa kashinda.Meneja Kimario amewataka wateja wapya na wazamani wa bank ya NMB kuendelea kuweka fedha kwenye akaunti zao mara kwa mara ili kujiweka katika nafasi ya kushinda bahati nasibu ya pata patia.
Mshindi wa shindano la pata patia linaloendeshwa na bank ya NMB matawi yote nchini Jofram Mohamed akizungusha gurudumu na kushinda shilingi laki 8 taslimu.
Mshindi mwingine wa shindano la pata patia linaloendeshwa na bank ys NMB kwa matawi yote nchini kutoka Mkoa wa Kagera Filbert Rogati akizungusha gurudumu na kushinda shilingi laki 4
Washindi wa shindano la pata patia wakisikiliza maelekezo toka kwa meneja wa NMB Mkoa wa Kagera kabla ya kuzungusha gurudumu la bahati nasibu
Baadhi ya wateja na wafanyakazi wa bank ya NMB tawi la bukoba mjini wakishuhudia washindi wanavyojipatia fedha zao kwa kuzungusha gurudumu.
MKUU WA WILAYA BUKOMBE AAGIZA MAAFISA TARAFA KUSIMAMIA HIFADHI YA MAVUNO KWA WANANCHI
Sunday, May 08, 2016
Maoni: 0
Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Mhe. Amani K. Mwenegoha ameagiza maafisa tarafa kusimamia kwa karibu shughuli za hifadhi ya mavuno yaliyopatikana katika Mvua za vuli Msimu wa 2015/2016 kwa kuhamasisha wananchi wenye mavuno mengi kila mahali kuhifadhi vizuri ili mavuno hayo yasiharibike na kuweka akiba ya kutosha kwaajili ya kaya zao.
Pia ameagiza Wakulima washauriwe kuuza ziada tu ya mavuno yao kwaajili ya kukidhi mahitaji yao muhimu na kila kaya isimamiwe kuhakikisha imehifadhi mazao ya chakula cha kuwatosha huku akiagiza Wafugaji washauriwe kuvuna sehemu ya mifugo yao kwaajili ya kukidhi mahitaji yao muhimu na kununua nafaka kwaajili ya kaya zao.
Amesisitiza maelezo haya yawafikie viongozi ngazi za kata,vijiji na vitongoji kwaajili ya utekelezaji na taarifa iwasilishwe kwa Mkuu wa Wilaya kabla ya 13/05/2016.
Imetolewa na
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Bukombe
Geita
06 Mei, 2016
TUZO ZA WANAFUNZI BORA AFRIKA MASHARIKI "ALL-STARS STUDENTS AWARDS"ZAANZISHWA
Sunday, May 08, 2016
Maoni: 0
Aaron Ally(Dj Aaron Tanzania)Mratibu wa‘All-stars Students Awards Akiongea Kwenye Kipindi cha Morning Trumpet kuelezea tuzo hizo.
Dj wa zamani wa Clouds FM, Aaron, yeye na Team yake(Ms Chiku Lweno, Mwl. Dany Mtanga) wameanzisha Tuzo walizoziita All-stars Students Awards.
Hizo ni tuzo zitakazotolewa kwa wanafunzi wa shule za sekondari A-level na O-level za Afrika Mashariki.Alhamisi hii Dj Aaron alialikwa kwenye kipindi cha Morning Trumpet cha Azam TV kuongelea tuzo hizo zitakazofanyika jijini Dar es Salaam.
Aaron amesema tuzo hizo zina dhumuni la kuwapa hamasa wanafunzi wa shule za Afrika Mashariki. Tuzo hizo zitatolewa kwa wanafunzi watakaofanya vizuri kwenye mitihani ya kidato cha nne na sita. pia na walimu husika ambao ni chachu ya wanafuzi ambao wamefanya vizuri kwenye hayo masomo.
Tuzo hizo zitaaangalia namba moja wote waliongoza katika nchi zote za Africa Mashariki,
Masomo yakayotolewa tuzo ni Kiswahili, Hesabu, Fizikia, Kemia, Bailojia na Kiingereza. Mchakato wa tuzo utaanza katikati ya mwezi wa sita.pia Special Talents, Michezo na Shule bora
UDONDOZI MAGAZETINI LEO
Sunday, May 08, 2016
Maoni: 0
MMOJA WA WAANZILISHI WA HIPHOP NCHINI AWA MUANDAAJI NA MTAYARISHAJI MZURI WA MUZIKI NJE YA TANZANIA
Sunday, May 08, 2016
Maoni: 0
Mmoja wa waasisi wa muziki wa kufoka foka nchini Chief Rhymson kutoka kundi la Kwanza Unit ambaye kwa sasa anafahamika kwa jina la Zavara ameendelea kufanya kazi zake za kimuziki katika eneo la uandaaji, uongozaji na kutengeneza video na hii moja ya kazi ya mikono yake inayozunguka duniani.
WABUNGE ,JAMES MBATIA NA JOSEPH SELASINI WATEMBELEA WAHANGA WA MAAFA YALIYOTOKANA NA MVUA ROMBO.
Sunday, May 08, 2016
Maoni: 0
Mbunge Mbatia akizungumza jambo mara baada ya kufika katika eneo lililokuwa na nyumba iliyobomoka baada ya kuporomokewa na kifusi na kusababisha kifo cha mtoto mmoja katika kijiji cha Manda juu wilayani Rombo.
Baadhi ya majirani wa familia iliyopoteza mtoto katika kijiji cha Manda wilayani Rombo baada ya nyumba aliyokuwemo mtoto kuporomokewa na kifusi kutokana na mvua kubwa zilizonyesha hivi karibuni.
Wabunge James Mbatia (Jimbo la Vunjo ) na Joseph Selasini wakiwa ofisini kwa Mkuu wa wilaya ya Rombo Lembris Kipuyo wakimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Maafa nchini Brigedia Jenerali Mbazi Msuya alipofika kutembelea wahanga wa mvua zilizonyesha hivi karibuni na kusababisha maafa.
Mbunge wa Jimbo la Rombo Joseph Selasini (kulia) akijaribu kutoa maelezo namna ambavyo wakazi wa kijiji cha Manda juu wilyani humo walivyo pata maafa yaliyotokana na kunyesha kwa mvua kubwa Aprili 24 na 25 mwaka huu.
Mbunge wa Jimbo la Vunjo ,James Mbatia akitoa pole kwa wakazi wa kijiji cha Manda juu wilayani alipokua akielekea kujionea namna ambavyo baadhi ya familia zilivyo athirika na mvua katika kjiji hicho na mtoto mmoja kupoteza maisha baada ya kifusi kuporomoka na kuangusha nyumba aliyokuwemo.
Mbunge wa Jimbo la Rombo ,Joseph Selasini (kushoto) akiongozana na Mkuu wa wilaya ya Rombo ,Lembris Kupuyo wakielekea kuijionea athari ya mvua hizo.
Read more »
TANZANIA UK DIASPORA TASKFORCE YATOA PONGEZI KWA DKT. ASHA ROSE MIGIRO
Sunday, May 08, 2016
Maoni: 0
SAKATA LA UFICHAJI SUKARI NCHINI,WAFANYABIASHARA KADHAA WABAINIKA SHERIA KUCHUKUA MKONDO WAKE.
Sunday, May 08, 2016
Maoni: 0
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa inafanya uchunguzi dhidi ya tuhuma zinazowahusu wafanyabiashara wa sukari nchini kwa kuficha bidhaa hiyo ili kusababisha upungufu katika soko na hivyo kuleta usumbufu kwa jamii ya watanzania wanaohitaji bidhaa hiyo kwa matumizi jambo ambalo limesababisha kupanda kwa bei hadi kufikia shilingi elfu nne kwa kilo moja ya sukari.
Taasisi imeanza uchunguzi dhidi ya Tuhuma hizi kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi na tayari tumeweza kutembelea Maghala ya mfanyabiasha Haruni Daudi Zacharia ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Al-Naeem yaliyoko Mbagala na Tabata ambaye ni miongoni mwa wafanyabiashara wakubwa nchini wa sukari na anayetuhumiwa kuficha bidhaa hii.
Mnamo tarehe 05 Mei, 2016 timu ya uchunguzi ilitembelea maghala ya Tabata na kubaini uwepo wa sukari yenye jumla ya tani 4,579.2 iliyonunuliwa toka Kiwanda cha Kilombero Sugar Company.
Aidha uchunguzi ulibaini kuwepo kwa njama za dhati za kutouza kwa sukari kulikofanywa na mfanyabiashara huyu kwani hata sehemu ya Maghala ilipo sukari hapa kuwepo dalili za upakiaji wa sukari na baada ya kufika Kitumbini tulibaini uwepo wa wananchi wengi waliokuwa wakihitaji bidhaa hiyo na wachache sana waliweza kuuziwa tena kwa kiwango kidogo sana kuliko mahitaji yao. Wananchi wengi walikosa huduma hiyo licha ya ukweli kwamba sukari ilikuwepo.
Uchunguzi uliofanyika umebaini kuwepo kwa mikakati ya dhati iliyokuwa ikifanywa na mfanyabiashar huyu kwa kununua sukari yote toka viwanda vya ndani na kisha kuihifadhi na kuuza bidhaa hiyo kidogo kidogo kwa wastani wa tani 250 kwa siku wakati alikuwa na uwezo wa kuuza zaidi jambo lililochangia uhaba wa sukari katika soko. Kuficha bidhaa ni kosa la uhujumu uchumi na ni kinyume na Aya ya 3 Jedwali la kwanza Sheria ya Uhujumu Uchumi Sura ya 200 [Chapisho la Mwaka 2002]. Serikali haitavumilia hujuma za namna hii na itachukua hatua kali dhidi ya mfanyabiashara yeyote ataekwenda kinyume na sheria hii.
Kuanzia sasa TAKUKURU inatoa wito kwa wafanyabiashara wote wa sukari kuacha vitendo vya kuficha sukari na vyombo vya uchunguzi vinafuatilia kote nchini na yeyote atakayebainika kufanya hujuma hizo atakabiliwa na mkondo wa Sheria.
VALENTINO MLOWOLA
MKURUGENZI MKUU WA TAASISI
YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA
7 MEI, 2016
MAKATIBU WAKUU WA VYAMA VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA WAKUTANA NCHINI ZIMBABWE
Sunday, May 08, 2016
Maoni: 0
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana akitoa mada kwenye Kongamano la siku Nne la Makatibu Wakuu wa vilivyokuwa Vyama vya Ukombozi Kusini mwa Afrika. Kongamano hilo linafanyika Victoria Falls Zimbambwe lilianza tarehe 4 – 8 Mei, 2016. Vyama hivyo ni ANC ya Afrika Kusini, FRELIMO ya Msumbiji, MPLA ya Angola, SWAPO Party ya Namibia na CCM ya Tanzania.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana akimpongeza Katibu Mtendaji Mkuu wa ZANU-PF Ndugu Ignatius Morgen Chombo kwa kufanikisha Kongamano la Makatibu Wakuu wa vilivyokuwa Vyama vya Ukombozi Kusini mwa Afrika na anaeshuhudia katikati ni Katibu Mkuu wa FRELIMO Ndugu Eliseu Machava. Kongamano hilo linafanyika Victoria Falls, Zimbabwe tarehe 4 – 8 Mei 2016
Picha ya pamoja ya Makatibu Wakuu wa vilivyokuwa Vyama vya Ukombozi Kusini mwa Afrika(FLM) wanaoshiriki Kongamano la siku Nne la kutafakari uimarishaji na uendelezaji wa ushirikiano wao na namna ya kukabiliana na changamoto walizonazo. Kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa ANC ya Afrika Kusini Ndugu Ndugu Gwede Mantashe, Katibu Mkuu wa FRELIMO ya Msumbiji Ndugu Eliseu Machava, Katibu Mkuu wa CCM ya Tanzania Ndugu Abdulrahaman Kinana, Makamu Waziri wa Uhusiano wa Kimataifa wa Chama cha Kikomnisti cha China (CPC) Ndugu Guo Yezhou, Katibu Mtendaji Mkuu wa ZANU-PF ya Zimbabwe Ndugu Ignatius Morgen Chombo, Katibu Mkuu wa MPLA ya Angola Ndugu Juliao Mateus Paulo na Katibu Mkuu wa SWAPO Party ya Namibia Ndugu Nangolo Mbumba. Kongamano hilo linafanyika Victoria Falls, Zimbabwe tarehe 4 – 8 Mei 2016.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana akibadilishana mawazo na Katibu Mkuu wa ANC ya Afrika Kusini, Ndugu Gwede Mantashe kwenye Kongamano la Makatibu Wakuu wa vilivyokuwa Vyama vya Ukombozi Kusini mwa Afrika(FLM) linalofanyika Victoria Falls, Zimbabwe tarehe 4 – 8 Mei 2016
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
RAIS DKT. MAGUFULI ATUNUKU KAMISHENI MAAFISA 586 KATIKA CHUO CHA MAAFISA WA JESHI MONDULI
Saturday, May 07, 2016
Maoni: 0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride kabla ya kutunuku Kamisheni kwa Maafisa Wapya 586 wa jeshi la Wananchi wa Tanzania kundi la 58/15 katika chuo cha kijeshi cha Monduli TMA mkoani Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride kabla ya kutunuku Kamisheni kwa Maafisa Wapya 586 wa jeshi la Wananchi wa Tanzania kundi la 58/15 katika chuo cha kijeshi cha Monduli TMA mkoani Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akitunuku kamisheni kwa maafisa wapya 586 wa jeshi la Wananchi wa Tanzania kundi la 58/15 katika chuo cha Mafunzo ya kijeshi cha Monduli TMA mkoani Arusha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Afisa Mpya wa cheo cha Luteni Usu, Nasra Rashid ambaye alifanya vizuri zaidi kuliko Maafisa Wanafunzi wanawake katika chuo cha kijeshi cha Monduli TMA mkoani Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya wananchi General Davis Mwamunyange mara baada ya kuwasili kwenye chuo cha Mafunzo Kijeshi cha Monduli TMA mkoani Arusha.
Maafisa Wanafunzi wakipita kwa mwendo wa haraka mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli kabla ya kutuniwa Kamisheni
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Monduli TMA Meja Jenerali Paul Peter Massao kabla ya kutunuku Kamisheni kwa Maafisa Wapya 586 katika chuo hicho cha Monduli.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa wapya aliowatunuku Kamisheni katika cha Mafunzo Kijeshi cha Monduli TMA mkoani Arusha. Wengine katika picha ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya wananchi Jeneral Davis Mwamunyange , Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Monduli TMA Meja Jenerali Paul Peter Massao, Waziri wa Ulinzi Dkt. Hussein Mwinyi pamoja na Maafisa wa ngazi za juu katika Jeshi la Ulinzi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi wa Ngarenaro waliomsimamisha wakati akitokea kwenye chuo cha Mafunzo ya Kijenshi cha Monduli mkoani Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akitembea kikakamavu mara baada ya kutoka kukagua gwaride katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Monduli TMA mkoani Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo wakati akizungumza na wanaanchi wa kona ya Mbauda mkoani Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Mkuu wa majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Monduli mara baada ya kutazama picha za Majenerali wastaafu waliongoza Jeshi la Wananchi katika miaka ya nyuma.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Mkuu wa majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Monduli mara baada ya kutazama picha za Majenerali wastaafu waliongoza Jeshi la Wananchi katika miaka ya nyuma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wakazi wa Kona ya Nairobi eneo la Arusha Tech mara baada ya kutoka kutunuku Kamisheni kwa maafisa Wapya katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Monduli mkoani Arusha. PICHA NA IKULU
NAIBU SPIKA ACKSON AFUNGUA SEMINA KWA WABUNGE KUHUSU UELEWA WA HAKI ZA WATU WENYE ULEMAVU
Saturday, May 07, 2016
Maoni: 0
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Wenye Ulemavu), Dk Abdallah Possi (kulia), akiwasilisha mada katika semina ya Wabunge kukuza na kuimarisha usawa wa watu wenye ulemavu nchini, kwenye Ukumbi wa Bunge wa Msekwa mjini Dodoma jana. Kutoka kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Bukene, Seleman Zedi (CCM) na Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson akifungua semina hiyo
Baadhi ya wabunge wakihudhuria kwenye semina hiyo
MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AFUNGUA MKUTANO WA BARAZA KUU LA UWT TAIFA DODOMA LEO
Saturday, May 07, 2016
Maoni: 0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia ngoma alipowasili katika Ofisi za Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM mjini Dodoma leo Mei 7,2016 kwa ajili ya kufungua mkutano wa Baraza Kuu la UWT Taifa.
Wajumbe wa Mkutano wa Baraza Kuu la UWT Taifa wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe. Samia Suluhu Hassan, alipokua akifungua Mkutano wa Baraza Kuu la UWT Taifa wenye lengo la kukumbushana katika majukumu ya kiutendaji kwenye ngazi mbalimbali za Jumuiya hiyo pamoja na kumpongeza Makamu wa Rais kwa kuchaguliwa Mwanamke wa kwanza katika Ngazi hiyo Kuu ya kitaifa. Mkutano huo umefunguliwa leo Mei 7,2016 katika Ukumbi wa Halmashauri Kuu ya CCM mjini.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Baraza Kuu la UWT Taifa wakimkabidhi zawadi za aina mbalimbali Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya kumpongeza kwa kuchaguliwa Mwanamke wa kwanza katika Ngazi Kuu ya kitaifa wakati wa Mkutano wa Baraza Kuu la UWT Taifa uliofunguliwa leo Mei 7,2016 katika Ukumbi wa Halmashauri Kuu ya CCM mjini Dodoma
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifungua Mkutano wa Baraza Kuu la UWT Taifa wenye lengo la kukumbushana katika majukumu ya kiutendaji kwenye ngazi mbalimbali za Jumuiya hiyo pamoja na kumpongeza Makamu wa Rais kwa kuchaguliwa Mwanamke wa kwanza katika Ngazi hiyo Kuu ya kitaifa. Mkutano huo umefunguliwa leo Mei 7,2016 katika Ukumbi wa Halmashauri Kuu ya CCM mjini Dodoma.
Wajumbe wa Mkutano wa Baraza Kuu la UWT Taifa wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe. Samia Suluhu Hassan, alipokua akifungua Mkutano wa Baraza Kuu la UWT Taifa wenye lengo la kukumbushana katika majukumu ya kiutendaji kwenye ngazi mbalimbali za Jumuiya hiyo pamoja na kumpongeza Makamu wa Rais kwa kuchaguliwa Mwanamke wa kwanza katika Ngazi hiyo Kuu ya kitaifa. Mkutano huo umefunguliwa leo Mei 7,2016 katika Ukumbi wa Halmashauri Kuu ya CCM mjini Dodoma.
Wajumbe wa Mkutano wa Baraza Kuu la UWT Taifa wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe. Samia Suluhu Hassan, alipokua akifungua Mkutano wa Baraza Kuu la UWT Taifa wenye lengo la kukumbushana katika majukumu ya kiutendaji kwenye ngazi mbalimbali za Jumuiya hiyo pamoja na kumpongeza Makamu wa Rais kwa kuchaguliwa Mwanamke wa kwanza katika Ngazi hiyo Kuu ya kitaifa. Mkutano huo umefunguliwa leo Mei 7,2016 katika Ukumbi wa Halmashauri Kuu ya CCM mjini Dodoma.
Mjumbe wa Mkutano wa Baraza Kuu la UWT Taifa Mama Lupembe akisalimiana na kumpongeza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuchaguliwa Mwanamke wa kwanza katika Ngazi Kuu ya kitaifa wakati wa Mkutano Mkuu wa UWT Taifa uliofunguliwa leo Mei 7,2016 katika ukumbi wa Halmashauri Kuu ya CCM Mjini Dodoma.
Makamu wa Raisv wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma Mhe. Adam Kimbisa kabla ya kufungua Semina ya Mafunzo kwa ajili ya kuwajengea Uwezo Viongozi na Mkada wa Chma cha Mapinduzi iliyofunguliwa leo Mei 7,2016 katika Ukumbi wa MORENA Mjini Dodoma. (Picha na OMR)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifungua Semina ya Mafunzo kwa ajili ya kuwajengea Uwezo Viongozi na Makada wa Chama cha Mapinduzi CCM iliyofunguliwa leo Mei 7,2016 katika ukumbi wa MORENA Mjini Dodoma.
akamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe. Samia Suluhu Hassan katikati akiwa bkatika picha ya pamoja na Viongozi na Makada wa Chama cha Mapinduzi CCM baada ya kufungua Semina ya Mafunzo kwa ajili ya kuwajengea Uwezo Viongozi na Makada wa Chama cha Mapinduzi CCM iliyofunguliwa leo Mei 7,2016 katika ukumbi wa MORENA Mjini Dodoma.
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment