N.I.H.F -KIKOA

N.I.H.F -KIKOA
N.I.H.F -KIKOA

FOREPLAN CLINIC

FOREPLAN CLINIC
FOREPLAN CLINIC

Sunday, May 15, 2016

WAFANYAKAZI WA BENKI YA EXIM WASHIRIKI KAMPENI YA USAFI DAR

MKUTANO WA WAZIRI UMMY MWALIMU ALIPOHUDHURIA MKUTANO WA VIONGOZI WANAWAKE KUHUS MASUALA YA AFYA

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akiongea na Wajumbe wa Mkutano wa Viongozi Wanawake katika masuala ya Afya katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Jijini Dar es Salaam 5 Mei, 2016.











SHIRIKA LA NDEGE LA NCHINI MAURITIUS LAZINDUA SAFARI ZA NDEGE ZA MAURITIUS KUJA DAR ES SALAAM.

RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AMUAPISHA DKT. ASHA-ROSE MIGIRO KUWA BALOZI WA TANZANIA NCHINI UINGEREZA










BENKI ya Rasilimali nchini (TIB) yatangaza mikopo yenye masharti nafuu kwa wakandarasi wazawa.

TIB Corporate Bank imesema imekusudia kuwawezesha kifedha wakandarasi wa ndani ili waweze kutekeleza vema majukumu yao ya kikandarasi.

Akizungumza wakati wa mkutano wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi nchini (CRB) uliofanyika jijini Mwanza, Mkuu wa Kitengo cha Mauzo ya Mikopo wa Benki ya TIB, Theresia Soka amesema benki yake imekuja na suluhisho la kutatua changamoto za wakandarasi wazawa.

TIB Corporate Bank imemua kurahisisha taratibu zake za kutoa mikopo kwa wakandarasi wa ndani kwa kuwataka kuwasilisha vielelezo tu vinavyomtambulisha kuwa amesajiliwa kisheria ili aweze kupata mkopo. ‘Tumeamua kurahisisha utaratibu wetu wa utoaji mikopo ili kuwawezesha wakandarasi na hivyo kuchangia ukuaji wa maendeleo nchini katika sekta hii muhimu ya ujenzi’ alisema Bi Soka.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa TIB Corporate Bahati Minja, alisema benki hiyo inayomilikiwa na Serikali, imeboresha huduma zake za kibenki ili kuwawezesha wakandarasi wazawa. ‘Lengo kubwa la Benki ya TIB Corporate ni kuhakikisha wakandarasi wanawezeshwa kifedha ili wawe na vitendeakazi vya ujezi’ alisema Bi Soka.

Hata hivyo wakandarasi waliohudhuria mkutano huo ambao miongoni mwao wamefadhiliwa na benki hiyo, waliupongeza uongozi wa Benki ya TIB Corporate kwa kuamua kuwawezesha kwa mikopo ya kikandarasi. Wakandarasi hao walisema uwezeshwaji huo wa mikopo nafuu inayotolewa na benki hiyo, itawasaidia kuendesha kampuni zao za ujenzi kwa ufanisi zaidi.

Mkutano huo wawakandarasi wenye kauli mbiu ya ‘Kuwajengea Uwezo Wakandarasi wa Ndani kwa ajili ya Uchumi Endelevu', utafuatiwa na mkutano mwingine utakaofanyika jijini Dar es salaam katika ukumbi wa Daimond Jubilee kuanzia tarehe 26 hadi 27 mwezi huu wa tano.

TIB Corporate Bank imefanya mabadiliko ya kitaasisi ili kuweza kuwa kituo cha huduma zote za kibenki kwa kushughulikia mahitaji ya wawekezaji wa ndani kwa lengo la kusukuma maendeleo ya 
Uchumi Endelevu: Changamoto na Mipango ya baadae’.

MAJALIWA:WANAVYUO WAFUATE TARATIBU NA SHERIA ZILIZOPO VYUONI










RITA yaanza kukusanya ada za Usajili kwa njia ya kielekroniki.













CCM YAKANUSHA TAARIFA ZILIZOTOLEWA KWA BAADHI YA VYOMBO VYA HABARI KUKUHUS KUKABIDHIANA KIJITI CHA UENYEKITI.



 Baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vinatoa taarifa potofu kuhusu mchakato wa Mwenyekiti wa sasa wa CCM Dkt. Jakaya Kikwete kukabidhi kijiti cha uongozi wa CCM kwa Rais John Pombe Magufuli kama ilivyo mila na desturi ya Chama Cha Mapinduzi. Yamekuwepo madai eti Mwenyekiti amekataa au anachelewesha kukabidhi kijiti.


Habari hiyo sio kweli kabisa na ni kinyume chake, kwani Dkt. Kikwete amekuwa akisisitiza kukabidhi madaraka mapema iwezekanavyo. Kwa ajili hiyo kwenye kikao cha Mei 3, 2016 alikataa kusiongezwe agenda nyingine ambazo zitalazimisha Mkutano Mkuu Maalum kuchelewa kufanyika kwa sababu ya kukamilisha maandalizi ya agenda hizo. Alisisitiza agenda iwe moja tu.

Dhamira ya kufanyika Mkutano Mkuu maalum mwezi Juni, 2016 iko pale pale. Kilichoelezwa kwenye kikao ni kutaka kukamilisha utaratibu wa kupata fedha za kugharamia mkutano huo. Taratibu zikikamilika tarehe itapangwa. Mipango ya kutafuta pesa inaendelea na ikikamilika tarehe itatangazwa.

Tunawataka wana-CCM wasihamanike wala kubabaishwa na taarifa za upotoshaji zinazofanywa na watu wenye nia mbaya na CCM. Hawa ni wale wale ambao wamekuwa wakiiombea mabaya CCM bila ya mafanikio.

Pia tunapenda kukanusha madai ati kuwa Mwenyekiti Kikwete aliwatahadharisha Wajumbe wa Kamati Kuu kuhusu ukimya wa Ndugu Edward Lowassa. Hakuna wakati wowote kauli kama hiyo aliitoa. Ni uzushi mtupu. Jina la Ndugu Lowassa halikutajwa kabisa.

Aidha, tunapenda kukanusha madai ya kufanyika mkutano baina ya Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Jamhuri ya Muungano, Makamu wa Rais na Katibu Mkuu wa CCM kuhusu uchaguzi wa Katibu wa Kamati ya Wabunge wa CCM. Hapajawahi kufanyika mkutano wa aina hiyo siku yoyote na mahali popote. Hivyo madai ya kuwepo kwa tofauti baina ya Viongozi wakuu kuhusu nani achaguliwe kuwa Katibu wa Wabunge wa CCM hayana msingi wowote. 

Kamati Kuu iliteua Wabunge wanne kugombea na kuwaachia Wabunge wa CCM kuamua. Kuhusisha Viongozi na hasa kuzua kuwepo kutokuelewana ni jambo la kusikitisha. Ni taarifa ya uongo yenye nia ovu kwa CCM na Viongozi wake.

Tunapenda kuwatahadharisha waandishi wa habari kuandika habari za ukweli. Waache kuzua mambo yenye kupandikiza chuki na mgawanyiko usiostahili kuwepo ndani ya CCM na kuyaeneza kwa watu. Waheshimu maadili ya kazi zao.

Napenda kuwahakikishia na kusisitiza kuwa hakuna mgogoro wa kukabidhi kijiti cha uenyekiti katika CCM na wala hautakuwepo.

Imetolewa na;
  
Ndugu Christopher Ole Sendeka   
                  MSEMAJI WA CCM                  
MJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,




05/05/2016

NJIA YA KIELETRONIKI YAANZA KUTUMIKA KUKUSANYA ADA ZA USAJILI.












PWANI: WIVU WA KIMAPENZI WASABABISHA KIFO KWA MAMA NA MTOTO








Wakazi wa Ilala wahakikishiwa usalama









UVCCM KULA SAHANI MOJA NA WALIOFUJA MALI ZAO








NHIF yazindua huduma Toto Afya Kadi







IFIKAPO 2030 WAKAZI WA DAR KUWA MILIONI 10.







ZIFF 2016 Announces Film Selection with Strong East African Presence











JK AKUTANA NA NAIBU MKURUGENZI WA GATES FOUNDATION YA MAREKANI

No comments:

Post a Comment

Blog Archive