MATUKIO BUNGENI DODOMA LEO
WATANZANIA WAHAMASISHWA KUJITOKEZA KUSHIRIKI SHINDANO LA KUONGEZA KIPATO
“Master Card Foundation inafanya kazi na mashirika yenye maono ili
kuleta zaidi upatikanaji wa elimu, mafunzo ya ujuzi na huduma za
kifedha kwa watu wanaoishi katika umaskini barani Afrika, ikiongozwa na
dira ya kuboresha mafunzo na kuongeza ushirikishwaji wa upatikanaji wa
kifedha ili kupunguza umaskini,” alisema Kivuti.
Kivuti alisema kuwa, kaya nyingi za vijijini barani Afrika
hazishirikishwi katika masuala ya kifedha na zaidi ya asilimia 70 za
familia Kusini mwa Jangwa la Sahara sehemu kubwa ya mapato yao
yanatokana na shughuli za kilimo, wakati huohuo watoa huduma za kifedha
wanakabiliana na changamoto kadhaa katika kuifikia jamii, hivyo Master
Card likaamua kusaidia miradi ambayo ina uwezo wa kuleta mabadiliko
chanya.
Aidha, Kivuti alitaja makundi yanayoruhusiwa kushiriki shindano hilo
kuwa ni pamoja na vikundi vya akiba, bima ndogo ndogo na mifumo ya umoja
wa fedha, fomu za maombi na mwongozo wa kushiriki shindano hilo
zinapatikana katika tovuti ya www.frp.org .
Jumla ya dola za Kimarekani milioni 10.6 zimetolewa kwa washindi wa
mwaka 2015 kwa ajili ya maendeleo Vijijini, kampuni zilizoshinda ni APA
Insurance Ltd kutoka Kenya, Finserve Afrika Ltd/Equitel kutoka Uganda,
M-KOPA LLC kutoka Tanzania, Musoni Kenya Ltd kutoka Kenya na Olam
Uganda Ltd kutoka Uganda. Kupitia kampuni hizo takribani watu milioni
nane wanaoishi maeneo ya Vijijini watakuwa na fursa ya kupata huduma za
kifedha ifikapo mwaka 2020
No comments:
Post a Comment