DAWASCO YATOA MKONO WA POLE KWA DADA ASHA CHANDE ALIYEPATA ULEMAVU WA MGUU WAKATI WA KUTAFUTA MAJI
Mkurugenzi
wa Sheria wa Mamlaka ya Maji Safi na Majitaka (Dawasco), Bernadetha
Mkandya akiwakatika picha ya pomoja na wafanyakazi wa(Dawasco),
leo,jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Sheria wa Mamlaka ya Maji Safi na Majitaka (Dawasco), Bernadetha
Mkandya akimkabidhi hundi ya sh mil 2.5 Dada Asha Chande Ramadhani ikiwa
ni sehemu ya kumpa pole kufuatia kupata ulemavu wa mguu wakati wa
harakati ya kutafuta maji .Dawasco imetoa mkono wa pole, Mchele Maharage
Unga wa Mahindi na Sukari pamoja na hundi ya Sh. Milioni 2.5.
Asha Chande Ramadhani akitoa neno la shukrani baada ya kupokea msaada wa kutoka Dawasco leo,jijini Dar es Salaam.
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA TANESCO LAZINDUA ''TANESCO HUDUMA
Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mhandisi Felchesmi
Mramba (kulia) akizungumza na Waandishi,viongozi wa Tanesco Dar es
Salaam jana wakati wa Uzinduzi wa 'Tanesco Huduma' zilizoboreshwa kwa
wananchi ,wateja wanaotumia simu za mkononi za kisasa katika mfumo
uliotengenezwa COSTECH.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mhandisi Felchesmi
Mramba (katikati) akizungumza.Wengine kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa
Tanzania Commission for Science and Technology (COSTECH),Hassan Mshinda
na Ofisa Mtendaji Mkuu wa DTBi,George Mulamula.
kiongozi wa Tanesco akizungumza.
MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AFUNGUA MKUTANO WA KUWEZESHA WANAWAKE KIUCHUMI KATIKA NCHI ZA UKANDA WA MASHARIKI NA KUSUNI MWA AFRIKA LEO
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akifungua mkutano kuhusu kuwezesha wanawake kiuchumi katika nchi za
Ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika. Mkutano huo umeandaliwa na
Jopo la Ngazi ya Juu la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon
aliloliteuwa Mwanzoni mwa huu, kusaidia kufanya uchambuzi na kutoa
mapendekezo ya namna ya kuchagiza kasi ya kuwezesha wanawake kiuchumi
ifikapo 2030. Umefanyika Leo April 29,2016 Hyatt Hotel Dar es salaam.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa
katika picha ya pamoja na Jopo la ngazi ya Juu la Katibu Mkuu wa Umoja
wa Mataifa la kuwezesha wanawake kiuchumi Baada ya kufungua mkutano
kuhusu kuwezesha wanawake kiuchumi katika nchi za Ukanda wa Mashariki na
Kusini mwa Afrika. Mkutano huo unazungumzia kuhusu kusaidia kufanya
uchambuzi na kutoa mapendekezo ya namna ya kuchagiza kasi ya kuwezesha
wanawake kiuchumi ifikapo 2030. Umefanyika Leo April 29,2016. (Picha na
OMR)
WAZIRI JENISTA ATEMBELEA BANDA LA MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI, KWENYE MAONYESHO YA USALAMA MAHALA PA KAZI
WAZIRI
wa NCHI ofisini ya WAZIRI Mkuu, Jenista Mhagama(wakwanza kulia), na
naibu wake, Dkt. Abdallah Possi.(wapili kulia), walipotembelea banda la
WCF, kwenye maonyesho ya Siku ya Usalama na afya mahala pa kazi mjini
Dodoma Aprili 28, 2016.Kushoto ni afisa uhusiano mwandamizi wa WCF,
Sebera Fulgence.WCF inashiriki maonyesho hayo yaliyoratibiwa na OSHA kwa
ushirikiano na TUCTA, ikiwa ni sehemu ya maadhimishi ya Siku ya
wafanyakazi Duniani(Mei Mosi).
Afisa uhusiano mwandamizi wa WCF, Sebera Fulgence, akizungumza kwenye maonyesho hayo ya OSHA.
Wananchi wakipatiwa MAELEZO kuhusu mafao ya fidia kwa wafanyakazi kutoka kwa maafisa wa WCF(kushoto).
MSTAHIKI MEYA WA MANISPAA YA KINONDONI AGAWA MAENO YA BIASHARA KWA WAFANYABIASHARA NDOGO NDOGO
Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Kinondoni Boniface Jacob akizungumzana wa
wafanyabiashara ndogo ndogo waeneo la Ubungo Stendi ya Mkoa kuhama
katika eneo hilo na kuhamia katika kituo cha mabasi Simu 2000, leo
jijini Dar es Salaam.
Wafanyabiashara
ndogo ndogo waeneo la Ubungo Stendi ya Mkoa wakijibapanga kwenye
maeneo yao waliypewa bure na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni
Boniface Jacob leo jijini Dar es Salaam.
Wafanyabiashara
ndogo ndogo waeneo la Ubungo Stendi ya Mkoa wakimsikiliza Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Kinondoni Boniface Jacob leo jijini Dar es Salaam.
(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii).
Meya wa
Manispaa ya Kinondoni Mhe. Boniface Jacob leo amefanya ziara katika eneo
la ubungo na kuongea na wafanyabiashara ikiwemo kuwaonyesha eneo la
kufanya biashara zao.
Amewataka
wafanyabiashara hao kesho wasiwepo maeneo hayo na kuwataka kuhamishia
biashara zao katika eneo la soko la Mawasiliano (Sinza), kwani
wasipofanya hivyo Kamati ya Ulinzi na Usalama Manispaa ya Kinondoni
imeshakaa na imepanga kuwaondoa.
Meya
alieleza kuwa isingekuwa busara kuwaondoa bila kuwaeleza watakwenda
wapi, Meya amewakabidhi wafanyabiashara hao kadi ambazo watazionyesha
ili wasisumbuliwe,pia amewataka wasilipe pesa yeyote endapo watatakiwa
walipie maeneo ya biashara waliyopewa.
Pia
amesema kuhusu ushuru hawatalipa kwa muda wa mwezi mmoja baada ya hapo
watalipia,Meya huyo amewahakikishia wafanyabiashara hao kuwa hakuna
atakayekosa eneo la kufanya biashara.
Afisa
biashara wa Manispaa ya Kinondoni amewataka wafanyabiashara hao
kutokaidi agizo hilo la Meya,hivyo kuanzia kesho wataondolewa kwa nguvu.
Meya
amesema kuna maeneo wamepewa madiwani akiwemo yeye na hayafanyiwi
biashara, hivyo sio sawa maeneo hayo wapewe wafanyabiashara.
TANAPA YAKABIDHI MABATI 2800 KUSAIDIA UJENZI WA MAABARA NA ZAHANATI WILAYANI SERENGETI
Mbunge wa
Jimbo la Serengeti Mhe. Marwa Ryoba (kushoto) akipokea msaada wa mabati
kutoka kwa Meneja Ujirani Mwema wa TANAPA Bw. Ahmed Mbugi wilayani
Serengeti.
Na Jacquiline Mrisho – Dar es Salaam
Shirika
la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limekabidhi jumla ya mabati 2800 kwa
Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti mkoani Mara kusaidia ujenzi wa
maabara 15 za shule za sekondari na zahanati zilizo katika Kata
mbalimbali za wilaya hiyo.Akikabidhi msaada huo Meneja ujirani mwema wa
Tanapa, Ahmed Mbugi amesema TANAPA imetoa msaada huo kusaidia Maendeleo
ya Elimu na Afya katika wilaya hiyo.“Mabati haya ni msaada ambao
tumeutoa kwa Wilaya ya Serengeti ikiwa ni muendelezo wa misaada
tunayoitoa kwa jamii hii ili kusaidia shughuli za maendeleo wilayani
hapa” alisema Mbugi.
Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, Naomi Nnko
aliongeza kuwa ujenzi wa maabara hizo kutawawezesha wanafunzi kusoma
masomo ya sayansi kwa vitendo, na hivyo kuongeza ufaulu katika shule za
sekondari wilayani humo.Aidha, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo,
Juma Keya alishukuru kwa msaada huo toka TANAPA na kuomba mashirika
mengine ndani na nje ya Wilaya ya Serengeti kushirikiana na Halmashauri
hiyo kuleta maendeleo katika jamii.
Akizungumza
katika hafla hiyo, Mkuu wa wilaya ya Serengeti, Maftah Mohammed
aliliomba shirika hilo kuchangia upatikanaji wa madawati katika shule za
msingi na sekondari zilizopo wilayani humo.Mpaka
sasa TANAPA imeisaidia Halmashauri hiyo kwenye ujenzi wa maabara katika
Kata ya Natta, uchimbaji wa marambo na ujenzi wa mabweni katika shule
za Sekondari.
Rais Magufuli afungua Kikao kazi cha makamanda Polisi na waendesha mashitaka awapa neno
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amelitaka Jeshi la Polisi nchini
na Ofisi ya Mwendesha Mashitaka kujirekebisha kwa kutekeleza wajibu wao huku
wakitanguliza maslahi ya taifa.
Rais Magufuli
ametoa maagizo hayo leo tarehe 29 Aprili, 2016 wakati akifungua kikao cha kazi
cha Makamanda wa polisi wa mikoa, Mawakili wafawidhi wa serikali wa Mikoa na Wakuu wa upelelezi wa Mikoa na
Vikosi, kinachofanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa Mikutano wa Dodoma
uliopo katika eneo la Tambukareli Mjini Dodoma.
Awali kabla ya
kutoa hotuba yake Rais Magufuli aliwapa nafasi Makamanda na Mawakili Wafawidhi
hao kutoa maoni yao juu ya changamoto zinazowakabili katika kutekeleza wajibu
wa kufanya upepelezi na kuendesha mashitaka, hususani kujua sababu za
kuchelewesha kesi za makosa ya jinai, ambapo wamedai ufinyu wa bajeti ndio
sababu kubwa ya kucheleweshwa kwa kesi za hizo.
Kufuatia kutajwa
kwa changamoto hiyo Rais Magufuli ameahidi kuhakikisha anawatafutia fedha kwa
ajili ya kukabiliana nazo, lakini ametaka fedha zitakazotafutwa zitumike vizuri
kwa kuwa taarifa zinaonesha Jeshi la Polisi limekuwa likihusishwa na matumizi
mabaya ya fedha hali inayoongeza ukubwa wa matatizo yanayokwamisha utendaji
wake wa kazi.
Ametolea mfano wa
taarifa za matumizi mabaya ya fedha zinazotolewa kwa ajili ya kununulia vifaa
na sare za askari, ama mikataba yenye mashaka inayotiwa saini kati ya Polisi na
wawekezaji kuwa ni baadhi ya mambo yanayoongeza hali ngumu ya utendaji kazi kwa
jeshi hilo.
"Oysterbay
pale ni eneo ambalo ni very prime, kila mmoja anajua, mmeingia kwenye mikataba
mnayoijua nyinyi, akapewa mtu anawajengea pale, sifahamu kama majengo hayo yanafaa.
Palikuwa na ubaya gani eneo la Oysterbay likawa na hati, mkaitumia hiyo hati
kwenda kukopa benki na kujenga nyumba hata za ghorofa 20 pale, mkaweka
investment na Polisi wenu wakakaa pale.
Nimesema lazima nizungumze kwa uwazi, nisiposema kwa uwazi nitajisikia vibaya
nikimaliza mkutano huu, nataka muelewe na muelewe ukweli
direction ninayoitaka mimi"
Amesema Rais Magufuli.
Aidha, Rais
Magufuli ameitaka Ofisi ya Mwendesha Mashitaka kujipanga kufanya kazi kwa
ufanisi na ameelezea kusikitishwa kwake na vitendo vya serikali kushindwa
katika kesi nyingi mahakamani licha ya kuwa na wanasheria mahiri.
"Niwaombe
mawakili na polisi wanaohusika na upelelezi mtangulize maslai ya nchi mbele,
kwa sababu kumekuwa na usemi kwa baadhi ya wapelelezi na mawakili wachache,
nasema wachache, panapokuwa na kesi inayohusiana na pesa pesa, wana misemo yao
wanasema dili limepatikana, na saa nyingine kesi inapopelekwa mahakamani
wana-collude Mawakili wa serikali na mawakili wanaomtetea mhalifu, na wanapo-collude siku zote serikali
inashindwa. Unapoona hali hiyo ya kila siku serikali inashindwa, halafu siku
hiyo unataka serikali ikuwezeshe, kwa vyovyote serikali inapata kigugumizi"
amesisitiza Rais Magufuli.
Dkt. Magufuli pia
amelitaka Jeshi la Polisi kujiepusha na kashfa ambazo zimekuwa zikisemwa dhidi
yake, ikiwemo maafisa wa Polisi kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya na
kuazimisha silaha kwa wahalifu wa ujambazi.Hata hivyo Rais
Magufuli amelipongeza Jeshi la Polisi na ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka kwa kazi kubwa wanayoifanya na
ametaka apelekewe mpango wa mahitaji yao ili atafute namna ya kuimarisha vyombo
hivyo.
Gerson
Msigwa
Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dodoma
29 Aprili,
2016
MATUKIO KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Ilala Azzan Mussa Zungu, bungeni mjini Dodoma Aprili 29, 2016.
Waziri
Mkuu,Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Ilemela na Naibu Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi, Angeline Mabula bungeni mjini
Dodoma Aprili 29, 2016.
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Mpwapwa, George Lubeleje kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Aprili 29, 2016.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Butiama , Nimrod Mkono
kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Aprili 29, 2016.
Bomba la mafuta kukamilika 2020
Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia
madini Profesa James Mdoe ( wa kwanza kushoto, waliokaa mbele); Naibu Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia nishati
Dk. Mhandisi Juliana Pallangyo ( wa pili
kushoto waliokaa mbele) pamoja na
wataalam wengine wa Wizara ya Nishati na
Madini wakifuatilia kwa makini hotuba
iliyokuwa inatolewa na Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini Nchini Uganda, Mhandisi Irene
Muloni (hayupo pichani) katika mkutano
kati ya nchi ya Tanzania na Uganda lengo likiwa ni kujadili mpango wa
ujenzi wa bomba la mafuta kutoka
Hoima, Uganda hadi katika bandari ya
Tanga nchini Tanzania.
Waziri wa Nishati na
Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akielezea uzoefu wa Tanzania kwenye
ujenzi wa miradi ya mabomba ya gesi na
mafuta katika mkutano huo. Kushoto ni Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini Nchini Uganda, Mhandisi Irene
Muloni na kulia ni Katibu Mkuu wa
Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa.
Wataalam kutoka
Wizara, taasisi na makampuni ya mafuta kutoka Tanzania na Uganda wakifuatilia
kwa makini mada iliyokuwa inawasilishwa na mwakilishi kutoka kampuni ya Total
katika mkutano huo.
Katibu Mkuu wa Wizara
ya Nishati na Maendeleo ya Madini
Nchini Uganda, Dk. Fred Kaliisa (kushoto)
akifafanua jambo katika kikao hicho.
Kulia ni Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini Nchini Uganda, Mhandisi Irene Muloni.
Waziri wa Nishati na
Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari
kuhusu utekelezaji wa mradi wa bomba la
mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi katika bandari ya Tanga nchini
Tanzania. Kulia ni Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini Nchini Uganda, Mhandisi Irene
Muloni.
Waziri wa Nishati na
Maendeleo ya Madini Nchini Uganda, Mhandisi Irene
Muloni (kulia) akifafanua jambo
alipokuwa akizungumza na waandishi wa
habari mara baada ya kukamilika kwa mkutano huo. Kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini,
Profesa Sospeter Muhongo.
Balozi wa Uganda Nchini
Tanzania, Dorothy Hyuha akifafanua jambo katika mkutano huo.
TANZANIA COMMENDED FOR ENHANCING GIRLS EDUCATION IN ICT.
The
Permanent Representative of Tanzania to the United Nations Economic
Commission for Africa (UNECA) and Ambassador of Tanzania to Ethiopia
H.E. Naimi Hamza Aziz(centre) poses for a picture with four student
girls from Tanzania who participated in the Girls in ICT Day
Celebrations in Addis Ababa under the auspices of International
Telecommunication Union ITU held at AU Headquarters yesterday.
From
left, Elida Alex Paul from Msalato Girls Secondary school, Dorice Mhanga
from Kleruu Secondary School in Iringa, Khudhaima Bedran Sultan from
Chasasa Secondary school in Pemba and Elician Yohana Kapi from Nyankumbu
Secondary school in Geita .(photo courtesy of Tanzanian Embassy in
Addis Ababa Ethiopia).
Tanzania
has been commended for its efforts in enhancing girl’s education in the
country including rural areas with the aim of achieving gender balance
by availing opportunities for girls to acquire skills in science and
technical subjects including Information and Communication Technology
(ICT).
The
compliments were given yesterday (April,28,2016) by the International
Telecommunication Union (ITU) Regional Director for Africa Mr. Andrew
Rugege when officiating at the opening ceremony of the International
Girls in ICT Day Celebration held at the African Union Headquarters in
Addis Ababa, Ethiopia.
“ Your
Excellency Tanzanian Ambassador Naimi Aziz, I would like you to convey
my regards to your government for its efforts in promoting ICT education
for girls as witnessed by four girls who travelled all the way from
Tanzania to join us in this auspicious occasion. The girls, excelled in
ICT competition organized by ITU,” he said praising the girls for
successful creating useful IT applications that could be used for
provision of social services.
The four
girl students from Tanzania who were invited for the occasion in the
Ethiopian capital, Addis Ababa include, Khudhaima Bedran Sultan from
Chasasa Secondary school in Pemba Zanzibar, Elician Yohana Kapi from
Nyankumbu Secondary school in Geita, Dorice Mhanga from Kleruu Secondary
school in Iringa and Elida Alex Paul from Msalato Girls Secondary
school in Dodoma.
Mr.
Rugege said ITU estimates a skills shortfall of over two million jobs in
the Information and communication technology (ICT) sector within the
next five years adding that, Girls and young women who learn coding,
apps development and computer science will not only be well-placed for a
successful career in the ICT sector, but ICT skills are rapidly
becoming a strong advantage for students in just about any other field
they might choose to pursue.
“ Girls
in ICT Day reminds us that ICTs help to improve the lives of people
everywhere and especially in Africa – through better health care, better
environmental management, better communications, and better educational
systems that transform the way children and adults learn,” he said
adding that the technology has been instrumental in creating job
opportunities to African youths.
The girls
participating in the school workshops were invited to the African Union
in Addis Ababa HQ for a half day celebration where they had the
opportunity to present their work and what they learned during the
workshops to the ITU officials, the diplomatic community, AU Staff and
ITU Delegates.
Six girls
from various secondary schools in Tanzania who excelled in ICT
competition coordinated by the ITU were invited for the ADDIS Girls in
ICT Day celebration having emerged winners from zonal and eventually
national ICT contests. Two of them could not travel to Addis Ababa to
join their colleague due to delay in visa application.
The Four Girls are scheduled to return home on Saturday.
ITU’s
Girls in ICT Day, is a global initiative aimed at raising awareness
among girls and young women about the importance of digital skills for a
successful professional career in all sectors and encouraging them to
consider studies and careers in Information and Communication
Technologies (ICT).
.ITU is the United Nations specialized agency for information and communication technologies – ICTs.
An
organization based on public-private partnership since its inception,
ITU currently has a membership of 193 countries and almost 800
private-sector entities and academic institutions. ITU is headquartered
in Geneva, Switzerland, and has twelve regional and area offices around
the world.
ITU
membership represents a cross-section of the global ICT sector, from the
world’s largest manufacturers and telecoms carriers to small,
innovative players working with new and emerging technologies, along
with leading R&D institutions and academia.
Founded
on the principle of international cooperation between governments
(Member States) and the private sector (Sector Members, Associates and
Academia), ITU is the premier global forum through which parties work
towards consensus on a wide range of issues affecting the future
direction of the ICT industry.
From Freddy Maro,
Tanzania Embassy Addis Ababa Ethiopia
NDUGAI AKABIDHI UENYEKITI WA JUKWAA LA MASPIKA WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI
Spika
wa Bunge Mhe. Job Ndugai akimkabidhi Uenyekiti wa Jukwaa la Maspika wa
Mabunge ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, Spika wa Bunge la
Afrika Mashariki Mhe. Daniel Kidega baada ya Tanzania kumaliza muda
wake. Alimkabidhi Uenyekiti huo wakati wa Mkutano wa kumi na moja (11)
wa Jukwaa la Maspika wa Mabunge ya nchi za Afrika Mashariki uliofanyika
Jijini Arusha leo tarehe 29 Aprili, 2016. Kulia ni Katibu wa Bunge Dkt
Thomas Kashililah
Spika
wa Bunge Mhe. Job Ndugai akisalimiana na Rais wa Bunge la Seniti la
Burundi Mhe Reverien Ndikuriyo wakati wa Mkutano wa Mkutano wa kumi na
moja (11) wa Jukwaa la Maspika wa Mabunge ya nchi za Afrika Mashariki
uliofanyika Jijini Arusha.
Spika wa Bunge Job Ndugai akisalimiana na Naibu Spika wa Bunge la Rwanda Mhe Jeanne Uwimanimpaye wakati wa Mkutano huo.Spika
wa Bunge Mhe. Job Ndugai (wa kwanza kulia) akifurahia jambo na Spika
wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Daniel Kidega (katikati) na Spika wa
Bunge la Kenya Mhe. Justin Muturi wakati wa Mkutano wa Mkutano wa kumi
na moja (11) wa Jukwaa la Maspika wa Mabunge ya nchi za Afrika Mashariki
uliofanyika Jijini Arusha.
Spika
wa Bunge Mhe. Job Ndugai amemkabidhi Uenyekiti wa Jukwaa la Maspika wa
Mabunge ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki Spika wa Bunge la Afrika
Mashariki Mhe. Daniel Kidega baada ya Tanzania kumaliza muda wake.
Spika
Ndugai alimkabidhi Uenyekiti huo wakati wa Mkutano wa kumi na moja (11)
wa Jukwaa la Maspika wa Mabunge ya nchi za Afrika Mashariki uliofanyika
Jijini Arusha leo tarehe 29 Aprili, 2016.
Mkutano
huo pia ulihudhuriwa na Spika wa Bunge la Seneti la Kenya, Spika wa
Bunge la Kenya, Rais wa Bunge la Seniti la Burundi, Naibu Spika wa Bunge
la Burundi, Naibu Spika wa Bunge la Rwanda, Spika wa Bunge la Afrika
Mashariki pamoja na Makatibu wa Mabunge ya nchi wanachama wa Afrika
Mashariki.
Akiukabidhi
Uenyekiti huo Spika Ndugai aliwashukuru Maspika wenzake kwa ushirikiano
walimuonesha katika kipindi chote cha Uongozi wake na kumtakia kila la
kheri Mwenyekiti mpya wa jukwaa hilo.
Maspika
wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki hushika Uenyekiti wa
Jukwaa la Maspika wa Jumuiya hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja ambapo
Tanzania ilichukua Uenyekiti wa Jumuiya hiyo mwaka jana.
Spika
wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe Kidega atashiki Uenyekiti wa Jukwaa
hilo kwa kipindi cha mwaka mmoja kabla ya kuukabidhi kwa Spika mwingine
katika mkutano ujao unaotarajiwa kufanyika nchini Kenya.
Pamoja
na mambo mengine mkutano huo wa Jukwaa la Maspika wa Mabunge ya nchi za
Jumuiya ya Afrika Mashariki ulijadili maswala mbalimbali yanayohusiana
na nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.Jukwaa la Maspika wa
Mabunge ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki lilianzishwa mwaka 2008.
Chama cha Wakunga Tanzania(TAMA) watoa mafunzo kwa wanahabari Nchini
Chama
cha Wakunga Tanzania (Tanzania Midwives Association-TAMA) imefanya
mkutano maalum wa kuhamasisha waandishi wa Habari kuhusu kazi za wakunga
katika kuelekea siku ya Wakunga Dunia ifikapo hapo Mei 5 mwaka huu.
Katika
mkutano huo uliofanyika jana Aprili 28, TAMA ilibainisha kuwa,
wanahabari wengi wamekuwa wakichanganya habari za wakunga wataalam
ambao wapo chini ya Chama hicho na wale wakunga wa jadi ambao hawana
taalum pamoja na kiapo cha kufanya kazi hiyo kitu ambacho kinaleta
usumbufu mkubwa kwa jamii.
Mratibu
wa TAMA, Bi. Martha Rimoy katika mkutano huo, ameeleza kuwa, shughuli
za Wakunga wataalam ni wale tu ambao wamesomea taaluma hiyo pamoja na
kula kiapo katika kumsaidia Mama na Mtoto na na huyo ndiyo anaitwa
Mkunga na si wale ambao hawajapata mafunzo wala kula kiapo.
Aidha,
aliomba wanahabari na vyombo vya habari kuzipatia nafasi/Kipaumbele
habari za Wakunga kwani zitaondoa woga kwa jamii iliyojenga Imani potofu
kwa wakunga.“Jamii
imekuwa ikijenga Imani potofu namna ya Wakunga buka kujua mkunga huyo
ni yupi. Tunaomba ifahamike Mkunga ni yule aliyepata mafunzo yake
kitaalam na pia kula kiapo pamoja na kusajiliwa na taasisi husika kama
ilivyo taratibu za Nchi.
Tuondoe
Imani zingine kwa Wakunga pia tunawaomba wanahabari kuweza kutoa elumu
ya kutosha kuhusiana na mambo ya Wakunga hasa wakunga wataalam ambao
wamepatiwa mafunzo yote ya kuhakikisha wanamuokoa Mama na mtoto wakati
wa uzazi” alieleza Bi. Martha Rimoy.
Kwa
upande wake Katibu Mkuu wa TAMA, Dkt Sebalda Reshabari ambaye alikuwa
mgeni rasmi katika mkutano huo, ameeleza kuwa, Wakunga wataalam wanao
wajibu wa
kumsaidia Mwanamke na mtoto katika kukabiliana na vifo vitokanavyo na
Masuala ya Uzazi vinavyozidi kuwatesa akina mama wengi, hasa inapokuja
wakati wa tendo la kujifungua.
Aidha,
Dkt. Sebalda amebainisha kuwa, pamoja na Changamoto mbalimbali, vifo
vya watoto walio chini ya umri wa miaka 5, imepungua kwa asilimia 81,
huku akitaka muendelezo wa elimu utolewe kwa Jamii.
Kwa
upande wake, Afisa Mipango wa Afya ya Mama na Uzazi wa Shirika la Idadi
ya Watu Duniani (UNFPA)nchini, Bi. Felista Bwana ameelezea kuwa, upo
umuhimu wa Mkunga mtalaam katika kuokoa Uhai wa Mama na mtoto kwani bila
wao Dunia ingekuwa kwenye matatizo makubwa.
Siku
ya Ukunga Duniani Inatarajiwa kuadhimishwa katika Viwanja vya Mnazi
mmoja Jijini Dar es Salaam, Mei 5 mwaka huu huku ikibeba ujumbe wa kauli
mbinu ya “Wanawake na Watoto wachanga ni muhimili wa Ukunga”.
Aidha,
mkutano huo ulieza changamoto wanazokabiliana nazo wakunga ni nyingi
hivyo wameimba Serikali kuangalia namna ya kukabiliana nayo ili kila
Mkunga kufanya kazi yake kwa uhuru na haki kwa dhama za sasa huku
wakiomba jamii kuondoa dhana potofu dhidi yao pindi wawaonapo katika
vituo vya Afya, Zahanati na Hospitali zote.
Mkutano
huo maalum wa TAMA, ulihusisha wanahabari mbalimbali kutoka katika
vyombo vya Habari nchini ikiemo, Magazeti, Radio, Televisheni na
magazeti ya mtandaoni.
Katibu
Mkuu wa TAMA, Dkt Sebalda Reshabari (kushoto) akieleza jambo kwa
wanahabari na watu mbalimbali (hawapo pichani) wakati wa mkutano huo kwa
waandishi wa habari juu ya kufahamishwa shughuli za Wakunga. Kulia ni
Bi. Felister Bwana kutoka UNPFA, Nchini Tanzania.
Mkutano huo ukiendelea...
Baadhi ya maafisa kutoka taasisi za Wakunga na mambo ya Afya wakifuatilia mkutano huo.
HALMASHAURI ZA MASASI, NANYAMBA KUANZA UTEKELEZAJI WA MRADI WA UIMARISHAJI MIFUMO SEKTA ZA UMMA AWAMU YA KWANZA MKOANI MTWARA
MKUU
wa Wilaya ya Newala, mkoani Mtwara, Christopher Magala akizungumza
wakati wa kuhitisha mafunzo ya utekelezaji wa Mradi wa Usimamizi wa
Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) yanayofadhiliwa na Shirika la Kimataifa la
Misaada la Marekani (USAID) na kutekelezwa katika Halmashauri 97 katika
mikoa 13 nchini. Uzinduzi wa mradi wa PS3 ngazi ya mkloa wa Mtwara
ilifanyika juzi mjini humo.
Mkoani
Mtwara mradi huo utatekelezwa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza
itahusisha Halamshauri ya Nanyamba na Halmashauri ya Wilaya Masasi.
Awamu ya pili ambayo itatekelezwa
mkoani mtwara kwa halamashauri saba zilizobaki utafanyika mwezi Februari na
Oktoba mwaka 2017 na utahusisha Halmashauri za Mjiwa Newala, Wilayaya Newala, Mji
wa Masasi, Wilaya ya Nanyumbu, Manispaa ya Mtwara, Wilaya ya Mtwara na Wilaya
yaTandahimba.
Baadhi
ya Maofisa wa Mradi wa PS3 pamoja na wakurugenzi wa Halmashauri za
Wilaya Mkoani Mtwara wakifuatilia ufungaji wa mafunzo hayo.
Washiriki wakifuatilia mada mbalimbali katika mafunzo hayo.
Mshauri wa Mradi katika Masuala ya Rasilimali Fedha, Dk Daniel Ngowi akizungumza wakati wa mafunzo hayo.
Kongamano la Uwekezaji Tanzania na Urusi lililofanyika jijini Dar
Makamu
wa pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali
Iddi akifungua kongamano la kujadili Fursa za Uwekezaji kati ya
Tanzania na Urusi lililofanyika jana jijini Dar es salaam ambalo
limewakutanisha wafanyabiashara mbalimbali wa Mataifa hayo mawili.
Waziri
wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akifafanua kwa
waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam kuhusu faida za ushirikiano
wa kibiashara kati ya Tanzania na Urusi utakaochangia maendeleo katika
sekta za Kilimo, Usafirishaji na Nishati hapa nchini.
Waziri
wa Viwanda na Biashara wa Urusi Mhe. Denis Manturov akizungumza kwenye
kongamano la kujadili fursa za Uwekezaji kati ya Tanzania na Urusi
lililofanyika jana Jijini Dar es salaam.
Baadhi
ya washiriki wa kongamano la kujadili fursa za Uwekezaji kati ya
Tanzania na urusi wakifuatilia mada wakati wa kongamano hilo jana Jijini
Dar es salaam.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali
Iddi (kushoto) akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta
Binafsi Tanzania Bw. Reginald Mengi jana Jijini Dar es salaam mara
baada ya kufungua kongamano la Uwekezaji kati ya Tanzania na Urusi.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali
Iddi (wanne kutoka kushoto) akiwa na Wawakilishi wa Serikali ya Urusi,
anayefuata ni Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Charles Mwijage
akifuatiwa na Waziri wa Viwanda Biashara na Masoko wa Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar Mhe. Amina Salum Ali.Picha zote na (Fatma Salum-
MAELEZO)
No comments:
Post a Comment