Sunday, May 27, 2012
Saturday, May 26, 2012
Thursday, May 24, 2012
BAADA YA JOHN MNYIKA KUIBUKA KIDEDEA MAHAKAMA KUU LEO
Mbunge wa jimbo la Ubungo CHADEMA Mh. John Mnyika akiwa amebebewa na
wanachama wa chama
hicho mara baada ya mahakama Kuu ya Tanzania kumtangaza mshindi katika
kesi ya uchaguzi iliyokuwa ikimkabili kesi ya kupinga matokeo ya
uchaguzi jimbo la Ubungo iliyofunguliwa na mpinzani wake Hawa Ng'humbi
wa chama cha
CCM.
Wafuasi wa chama hicho wakiwa wamefurika katika mahakama kuu ya Tanzania leo kusikiliza hukumu ya John Mnyika
Wafuasi wa CHADEMA wakishangilia katika mahakama kuu ya Tanzania leo mara baada ya hukumu ya John Mnyika kutolewa leo
Jeshi la polisi likiwa kwenye msafara kusindikiza maandamano ya chama
hicho kuelekea katika njimbo Ubungo mara baada ya ushindi huo
Kijana ambaye hakujulikana jina lake akiwa amebebwa baada ya kuanguka kwenye pikipiki
Johni Mnyika akionyesha ishara ya ushindi akiwa na wapambe wake pepembeni wakielekea Ubungo kwa ajili ya mkutano wa hadhara
Hapa safari imenoga wakielekea katika jimbo la umbungo
Waandishi wa habari wakiwa kwenye kupata habari walipowasili katika jimbo la John Mnyika.
John mnyika akiutubia wafuasi wa chama chake katika jimbo lake la Ubungo mara baada ya kuwasil.
Wednesday, May 23, 2012
Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Yapitia Ripoti ya Sheria Zinazosimamia Mfumo wa Haki za Madai
Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania
Buxton Chipeta akitoa ufafanuzi wakati wa mkutano wa kupitia Ripoti za Sheria
zinazosimamia Mfumo wa Haki za Madai jijini Dar es Salaam.
Washiriki wa Mkutano wakimsikiliza Jaji Mstaafu Chipeta
Na Munir Shemweta
Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania imeanza kupitia ripoti za Mapitio ya Sheria zinazisimamia mfumo wa haki za Madai kwa lengo la kufanya maboresho ya sheria hizo.
Katika Mapitio hayo Tume kwa kushirikiana na wadau ambao ni wakufunzi wa vyuo, Taasisi zinazotoa misaada ya kisheria, Wanasheria, Mawakili na Mahakimu kwa pamoja itapitia ripoti zilizofanyiwa kazi na Wataalamu washauri.
Katika mchakato huo Tume imegawa makundi manne yatakayopitia ripoti hiyo katika mikoa ya Mwanza ambapo kundi hilo linaongozwa na Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Profesa Ibrahim Juma, Arusha Kamishna wa Tume Ester Manyesha, Mbeya Kamishna wa Tume Profesa Sufian Bukurura, Dodoma Kamishana Ernest Mwipopo na Dar es Salaam linaloongozwa na Jaji Mstaafu Praxon Chipeta..
NMB NA SERENGETI ZAICHANGIA TWIGA STARS MILIONI THELATHINI
Katika
kuendeleza soka Tanzania, leo hii Benki ya NMB kwa kushirikiana na kampuni
ya Bia ya Serengeti imesaidia maandalizi ya Twiga Stars kwa kutoa
jumla ya shilingi Milioni Thelathini. Pia NMB na Serengeti wamekabidhi
vifaa vyenye thamani ya Milioni Tano kwa timu hiyo ya Twiga
Stars.
Akizungumza wakati wa
makabidhiano hayo, Mkuu wa idara ya Masoko na Mawasiliano wa NMB Bw.
Imani Kajula alisema; “NMB imekua
mbele katika kuchangia soka Tanzania, leo hii NMB ikishirikiana
na Serengeti tunachangia maandalizi ya Twiga Stars”.
NMB inatambua kuwa Twiga
Stars ikiwezeshwa inaweza ikafanya vizuri zaidi. Ili kutimiza lengo
hili, NMB Ikiwa ndiyo benki yenye mtandao mpana wa matawi mengi
Tanzania nzima pia imeanzisha akaunti maalum kwa ajili ya kuchangia
Twiga Stars. Yeyote atakayeguswa kuchangia Twiga Stars anaweza kuchangia
kupitia akaunti namba 22310001185 yenye jina CHANGIA TWIGA STARS ACCOUNT
Naibu Mkurugenzi wa michezo, Bi. Juliana Yasoda
(kulia) akipokea vifaa vya michezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Masoko
wa Serengeti, Bw. Ephraim Mafuru (kati) na Mkuu wa Idara ya
Masoko na Masiliano wa NMB, Bw. Imani Kajula (Kushoto). Wanaoshuhudia
tukio hilo ni Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),
Bw. Sunday Kayuni (pili kushoto) na kocha msaidizi wa Twiga Stars Bi.
Nasra Mohamed.
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia January Makamba atembelea Makao Makuu ya Vodacom Tanzania
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia January Makamba
akizungumza na watendaji wakuu wa kampuni ya Vodacom (hawapo pichani)
wakati alipotembelea makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es salaam
katika ziara maalum ya kujifunza shughuli za mawasiliano nchini. Kulia
na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza.
MARC, MARAS, MADC WAONYWA KUWA WAADILIFU
Wito
huo umetolewa leo (Jumatano, Mei 23, 2012) katika mada tatu zilizowasilishwa
leo kuhusu maadili kwa viongozi wa umma kwenye mafunzo
maalum ya siku 10 kwa Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala na Wakuu wa Wilaya.
Mafunzo hayo ambayo leo yamefikia siku ya tatu yanafanyika kwenye ukumbi wa St.
Gaspar mjini Dodoma.
Akitoa mada kwa viongozi hao, Kamishna
wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji (Mst.) Salome Kaganda
alisema uadilifu ni zaidi ya kuzingatia sheria, taratibu na kanuni na akawataka
viongozi hao kuonyesha njia kwa matendo na mwenendo mwema ili waweze
kuwasimamia watendaji walio chini yao.
Naye Askofu Mkuu Mstaafu, Mhashamu
Donald Mtetemelwa aliwataka washiriki wa mafunzo hayo kujiepusha na matumizi
mabaya ya mamlaka walinayo kwani wasipofanya hivyo wanaweza kujikuta
wakiwaumiza wengi. “Lengo la kiongozi ni kubeba maumivu ya watu na siyo kupeleka
maumivu kwa wananchi,” alisema.
Alisema Tanzania kwa sasa inakabiliwa
na tatizo la kukosa viongozi wengi walio waadilifu kwa sababu wengi wao
wamemuacha Mungu kwa kisingizio cha kuwa na majukumu mengi. “Watu wakipewa
madaraka wanajitenga na Mungu, lakini lazima wakumbuke kuwa uadilifu wao utategemea
ni kwa kiasi gani wanamcha Mungu,” aliongeza.
WAFANYABIASHARA NDOGONDOGO WAIOMBA SERIKALI KUWATENGEA SOKO MAALUM ILI KUEPUKA ADHA INAYOWAKUMBA
WAJASIRIAMALI wadogo wameiomba serikali
kuwatengea soko maalumu ili waondokane na adha mbalimbali wanazokumbana nazo,
ikiwemo ya kutojulikana kwa bidhaa zao.
Wakizungumza na waandishi wa habari jijini
Dar es Salaam jana, kwenye Maadhimisho ya siku ya Afrika walisema licha ya
kukabiliwa na changamoto mbalimbali hususan katika kutangaza bidhaa zao, lakini
bado jamii imeshindwa kuziamini bidhaa zao kutokana na kutokuwa na nembo ya
ubora, ‘TBS’.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake Juliana
Massawe alisema kuwa mbali na wajasiriamali hao kuendesha biashara zao katika
mazingira magumu, lakini wanakabiliwa na tatizo la kutokuwa na nembo maalumu
inayotambulisha bidhaa zao kama zina ubora unaotambulika, jambo ambalo huwalazimu
kutoa elimu kwa wateja kabla ya kuwauzia.
Aidha, alilitaja baadhi ya
changamotozinazowakabili ni jinsi ya upatikanaji wa vifungashio ambapo kwa sasa
vinapyikana kwa gharama kubwa.
“Unajua hivi sasa tuko katika wakati mgumu
wa upataji wa vifungashio, ukweli kwamba wachina wanapovikisha hapa bei yake
inakuwa hali inayotulazimisha kupandisha gharama ya bidhaa zetu ili tupate
faida”alisema Masawe.
Magesa Amani alitoa wito kwa watanzania
kujenga ustaarabu wa kununua bidhaa zinazotengenezwa nchini kwani zina ubora
ukilinganisha na baadhi ya zile zinazotoka nje.
Naye Mratibu wa maadhimisho hayo, Deus
Stevin alisema kuwa maadhimisho hayo ufanyika kila mwaka 26 Mei kwa lengo la
kumbukumbu ya uhuru wa Mwafika.
Vile vile Stevin alikiri kuwepo kwa tatizo
la vifungishio pamoja na soko maalumu, ila akasema kwa sasa wameandaa mfumo wa
kutoa elimu kwa wajasiriamali kabla hawajaangalia mtaji ili kumuandaa kwa ajili
ya ubunifu wa bidhaa zenye ubora.
“Kabla hatujaangalia mtaji, tunaangalia
ubora wa bidhaa yenyewe kwa lengo la kudhibiti, hata hivyo tunatoa na elimu ya
mafunzo, soko la pamoja pamoja na usafi wa kufunga bidhaa” alifafanua Stevin.
Hata hivyo alifafanua kuwa tatizo la
vifungishio si kwa wajasiriamali wa mjini tu, bali tatizo hilo linawakabili
hata wale wa vijijini, hivyo kuna haja ya serikali kuangalia namna ya kutafuta
wadau mbalimbali ili kukabiliana na tatizo hilo sugu.
Kilele cha maadhimisho hayo kitafanyika Mei
26 katika viwanja vya mnazi mmoja na kufungwa na waziri wa Biashara,viwanda na
masoko Abdallah Kigoda.
MKAZI WA JIJI APANDISHWA KIZIMBANI KWA UNYANG'ANYI
MKAZI wa jijini Dar es Salaam Humphery Mwankemwa amepandishwa
kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala kwa kosa la kutumia nguvu
na kuiba mali yenye thamani ya sh.milioni 112.9 katika ubalozi wa Sudan
nchini Tanzania.
Mwendesha Mashtaka wa
serikali,Aidah Kisumo alidai mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo
Tarsila Kisoka alidai kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo Mei 6
eneo la Ubalozi wa Sudan barabara ya Ally Hassan Mwinyi jijini Dar es
Salaam.
Alisema kuwa Mwankemwa
aliiba fedha taslimu sh. milioni 7.2 na dola za Kimarekani 71000,
ambazo fedha zote hizo zina thamani ya sh milioni 112.9.
Baada ya kusomewa
mashitaka hayo mshitakiwa alikana kosa na kurudishwa rumande kwa
kushindwa kukidhi masharti ya dhamana na kesi itatajwa tena Julai 6
mwaka huu.
WANANCHI WENYE HASIRA WAUWA MAJAMBAZI WATATU JIJINI ARUSHA
NA GLADNESS MUSHI -ARUSHA
WANANCHI wenye hasira katika eneo la Ngusero Ndani ya
manispaa ya Arusha wamewaua majambazi matatu kwa silaha za jadi mara baada ya
majambazi hayo kubainika kuwa wanapanga mbinu mbalimbali za kuvunja nyumba
Akiongea na waandishi wa habari mapema leo kamanda wa polisi
wa mkoa wa Arusha Bw Thobias Andengenye alisema kuwa tukio hilo
lilitokea alfajiri ya saa kumi za asubui ambapo majambazi hayo yalifika katika
eneo hilo huku
yakiwa ndani ya gari
Kamanda Andengenye alisema kuwa mara baaada ya majambazi
hayo kufika katika eneo hilo la tukio wakiwa na
gari aina ya Corola lenye namba T830 AHU walianza kuzunguka zunguka katika eneo
hilo ili
kupanga nyumba ambayo wanaingia hali ambayo iliwashitua wananchi
Alifafanua kuwa mara baada ya wananchi kutilia shaka gari hilo
ambalo lilikuwa na majambazi hao waliamua kuwaweka chini ya ulinzi na kukagua
gari hilo ambapo walikutana na Silaha za jadi
pamoja na silaha nyingine ambazo ni za kuvunjia nyumba hali ambayo ilisababisha waweze
kupigwa sana na wananchi hao
“inavyosemekana ni kwamba hawa majambazi walikuwa
wameshazunguka san a na gari lao kwa muda mrefu sana na sasa mara baada ya
kuhisiwa wananachi waliamua kujichukulia sheria mkononi na kisha kuanza
kuwapiga sana hali ambayo ilisababisha Mauti yao hapo hapo”alisema kamanda
Andengenye.
Aliongeza kuwa mara baada ya Jeshi la Polisi kufika katika
eneo hilo waliweza kugundua kuwa kati ya
majambazi hayo matatu mawili yalikuwa yanatafutwa na jeshi hilo bila mafanikio kwa kuwa walikuwa
wanatuhumiwa kwa makosa ya unyanganyi wa kutumia silaha ndani ya maeneo
mbalimbali ya Mji wa Arusha
Mkazi wa Arusha ashinda piki piki bahati nasibu ya Simba
Mwandishi wetu
SHABIKI
wa timu ya soka ya Simba mkoani Arusha, Abubakar Hamis ameibuka kidedea
katika droo ya bahati nasibu katika kampeni ya changia simba
inayoendeshwa kwa ushirikiano baina ya Kampuni ya Push Mobile Media na
klabu ya Simba.
Katika
bahati nasibu hiyo Hamis ambaye ni dereva taxi amejinyakulia zawadi ya
pikipiki yenye thamani ya zaidi ya shilingi milion tatu.
Kwa
mujibu wa Meneja Kampeni wa Simba sms, Talib Rashid shabiki huyo ni
miongoni mwa mashabiki zaidi ya 40 wa klabu hiyo kongwe hapa nchini
waliojishindia zawadi mbalimbali ikiwamo pesa taslimu.
"Droo
kubwa itafanyika Julai na mshindi atajinyakulia bajaji," alisema Rashid
na kuongeza mashabiki wanatakiwa kuandika neno Simba na kutuma kwenda
15678 kuingia katika bahati nasibu hii.
Afisa
Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga alisema ushindi wa shabiki huyo ni
uthibitisho tosha kwamba mashabiki wao wanashinda katika bahati nasibu
hiyo.
"Naomba
wanachama na mashabiki wetu wajitokeze kushiriki katika bahati nasibu
hii kwani ni moja ya kuichangia klabu ya Simba iweze kujiendesha na
kufanya vizuri zaidi ndani na nje ya Tanzania," alisema Kamwaga.
Mshindi
atazawadiwa zawadi yake ndani ya wiki mbili kuanzia sasa na kampuni ya
Push Mobile Media itagharimia gharama za usafiri na kulala wakati wa
kuja hapa jijini.
Alisema kuwa kwa sasa wamebakiza piki piki moja na bajaj ambazo drow yao itachezeshwa siku moja.
WAHINDU WA DHEHEBU LA SWAMINARAYAN WAFANIKIWA KUWATIBU WATOTO ELFU 17 KILA MWAKA NA KUWAPA MSAADA WANAFUNZI 4000 KILA MWAKA
BAADHI YA WANANCHI WA MJI WA ARUSHA WAKIWA KWENYE MSIKITI WA KITALII ULIOJENGWA NA WAHINDU
NA GLADNESS MUSHI -ARUSHA
Zaidi ya watoto elfu kumi na saba pamoja na wanafunzi 4000
ambao wanatokea katika mazingira magumu kila mwaka wanafanikiwa kupewa misaada
mbalimbali ya kujikimu na Masomo huku watoto waliowagonjwa nao wanapewa msaada
wa matibabu bure mpaka waweze kupona
Akiongea na waandishi wa habari mapema leo mwenyekiti wa
Dhehebu la Swaminarayan ambao waumini wake wengi wanaasili ya kihundu,Bw Subash
Patel alisema kuwa lengo ni kuwasaidia na kuwakomboa watoto wa kitanzania
Bw Subash alifafanuwa kuwa hali hiyo imekuja mara baada ya
kuona kuwa watoto hao wana umuhimu mkubwa sana
kwa jamii na pindi wanapokosa huduma za kielimu au matibabu imara basi huwa
wanapoteza haki zao za msingi
TANZANIA YADHAMIRIA KUWEKA MAZINGIRA YA UPATIKANAJI WA MSAADA WA KISHERIA.
Mratibu
Mkazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania, Dk. Alberic Kacou akizungumza
wakati wa ufunguzi wa warsha ya Mpango wa Msaada wa Kisheria Barani
Afrika iliyoandaliwa na UNDP.
Dk. Kacou amesema warsha hii ya Msaada wa Kisheria ni
hatua nyingine katika kuelekea kuondoa vikwazo katika uwezeshaji wa
Kisheria na kupatikana kwa haki kitu ambacho kimeathiri kwa kiwango
kikubwa bara hili katika nyanja mbalimbali ikiwa ni pamoja na maisha ya
watu, mali, Uraia, huduma za kijamii na kukosekana kwa fursa za
maendeleo. Kulia ni Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mh.
Angela Kairuki
Dk. Kacou amesema warsha hii ya Msaada wa Kisheria ni
hatua nyingine katika kuelekea kuondoa vikwazo katika uwezeshaji wa
Kisheria na kupatikana kwa haki kitu ambacho kimeathiri kwa kiwango
kikubwa bara hili katika nyanja mbalimbali ikiwa ni pamoja na maisha ya
watu, mali, Uraia, huduma za kijamii na kukosekana kwa fursa za
maendeleo. Kulia ni Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mh.
Angela Kairuki na kushoto ni mmoja wa maafisa wa makao makuu ya UNDP New
York Shelley Inglis.
Mgeni
rasmi Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Angela Kairuki akisoma
hotuba wakati akifungua rasmi warsha ya Mpango wa Msaada wa Kisheria
Barani Afrika iliyoandaliwa na UNDP na kuhudhuriwa na wadau wa masuala
ya sheria kutoka mataifa mbalimbali barani Afrika wakiwemo wenyeji
Tanzania.
Katia
ufunguzi huo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam Mh. Kairuki amesema
Serikali ya Tanzania imefanya jitihada mbalimbali za kuboresha huduma za
misaada ya Kisheria haswa kwa watu ambao ni vigumu kuupata msaada huo,
ambao wengi wao wanaishi katika maeneo ya vijijini.
Kauli mbiu ya Warsha hiyo ni " Taking Forward Legal Aid Programming in Africa: Experiences and Lessons in Policy and Programming".
Baadhi
ya wadau wa masuala ya sheria kutoka mataifa mbalimbali barani Afrika
wakiwemo wenyeji Tanzania wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi Mh. Angela
Kairuki.
Miss Kigamboni City 2012 waanza kujinoa
Na Mwandishi Wetu
MAZOEZI kwa ajili ya kushiriki shindano la kumsaka malkia wa kitongoji cha Kigamboni mwaka huu 'Miss Kigamboni City 2012' yameshaanza mapema wiki hii imefahamika.
Shindano hilo limepangwa kufanyika ifikapo Juni 15 kwenye ukumbi wa Navy Beach ulioko huko Kigamboni hapa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza leo jijini, Mratibu wa shindano hilo, Somoe Ng'itu, alisema kuwa maandalizi ya kinyang'anyiro hicho yanaendelea na warembo tayari wameshaanza mazoezi kwenye ukumbi wa Break Point ulioko Posta jirani na Club Billicanas.
Alisema kuwa bado milango iko wazi kwa warembo wenye sifa kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini wanakaribishwa kushiriki kuwania taji hilo.
Aliongeza kuwa kampuni yake imejipanga kuhakikisha shindano la mwaka huu linakuwa bora na kuwapata washiriki watakaokwenda kutwaa taji la Kanda ya Temeke na hatimaye taji la taifa la Redd's Miss Tanzania baadaye mwaka huu.
"Kila kitu ni maandalizi, tumejiandaa katika kufanya mchakato wa kupata warembo wenye sifa ili waweze kwenda kuiwakilisha vyema Kigamboni katika mashindano ya Kanda," alisema Somoe.
Aliwataja warembo ambao wameshaanza mazoezi kuwa ni pamoja na Caroline Peter, Theopisther Wenso, Sophia Martime, Amina Aboubakar, Aisha Rajab, Rosemary Peter, Mariam Mbulilo, Julieth Phili na Doreen Kweka.
Warembo hao wanafanya mazoezi chini ya Hawa Ismail ambaye alikuwa mshindi ya shindano la Kanda ya Temeke mwaka 2003.
"Bado tunakaribisha wadau wa sanaa ya urembo kutudhamini shindano hili, tunaamini uwepo wao ndio utafanikisha ubora na hadhi ya shindano letu mwaka huu kama tulivyodhamiria," aliongeza.
Aliwataja wadhamini ambao tayari wamethibitisha kudhamini shindano hilo ni pamoja na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Redd's, Dodoma Wine na NSSF.
Taji la taifa la shindano hilo linashikiliwa na Salha Israel ambaye alitokea katika Kanda ya Ilala.
Makao Makuu ya Benki ya Azania kuhamia Mawasiliano Towers
Na Mwandishi Wetu
UONGOZI wa benki ya Azania umeridhia uhamisho wa makao makuu ya benki hiyo kutoka Masdo House, mtaa wa Samora jijini Dar es Salaam kwenda jengo la Mawasiliano Towers iliyopo mkabala na barabara ya Sam Nujoma kuanzia Jumatatu wiki ijayo kwa lengo la kuwatumikia wateja wa benki hiyo katika mazingira yenye nafasi ya kutosha.
Hata hivyo, tawi la Masdo litaendelea kuwahudumia wateja waliopo katikati ya Jiji huko makao makuu mapya ya benki hiyo yaliyopo Mawasiliano Towers yakitoa huduma za kibenki kwa maeneo yaliyopo karibu na Ubungo, Mwenge ,Sinza na mengineyo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na uongozi wa benki hiyo kwa vyombo vya habari jana, benki ya Azania itaendelea na mpango wake wa kujiimarisha zaidi kwa kuendelea kufungua matawi zaidi nchini ikiwa na lengo la kusogeza huduma za kifedha karibu na watu na pia kuhakikisha usalama kwa pesa zao.
Kupitia taarifa hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Charles Singili alisema benki yake ipo mbioni kufungua tawi jingine jipya katika Wilaya ya Geita na maeneo mengine yakiwemo Lamadi, Katoro na Kagongwa ifikapo mwisho wa mwezi ujao, hatua ambayo itasaidia kuimarisha uwepo wa benki hiyo katika kanda ya ziwa.
"Tunatarajia kufungua matawi mengine zaidi nchi nzima ifikapo mwisho wa mwaka huu ambayo yatasaidia benki yetu kuwa kitovu cha huduma za kifedha kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati nchini.
UONGOZI wa benki ya Azania umeridhia uhamisho wa makao makuu ya benki hiyo kutoka Masdo House, mtaa wa Samora jijini Dar es Salaam kwenda jengo la Mawasiliano Towers iliyopo mkabala na barabara ya Sam Nujoma kuanzia Jumatatu wiki ijayo kwa lengo la kuwatumikia wateja wa benki hiyo katika mazingira yenye nafasi ya kutosha.
Hata hivyo, tawi la Masdo litaendelea kuwahudumia wateja waliopo katikati ya Jiji huko makao makuu mapya ya benki hiyo yaliyopo Mawasiliano Towers yakitoa huduma za kibenki kwa maeneo yaliyopo karibu na Ubungo, Mwenge ,Sinza na mengineyo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na uongozi wa benki hiyo kwa vyombo vya habari jana, benki ya Azania itaendelea na mpango wake wa kujiimarisha zaidi kwa kuendelea kufungua matawi zaidi nchini ikiwa na lengo la kusogeza huduma za kifedha karibu na watu na pia kuhakikisha usalama kwa pesa zao.
Kupitia taarifa hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Charles Singili alisema benki yake ipo mbioni kufungua tawi jingine jipya katika Wilaya ya Geita na maeneo mengine yakiwemo Lamadi, Katoro na Kagongwa ifikapo mwisho wa mwezi ujao, hatua ambayo itasaidia kuimarisha uwepo wa benki hiyo katika kanda ya ziwa.
"Tunatarajia kufungua matawi mengine zaidi nchi nzima ifikapo mwisho wa mwaka huu ambayo yatasaidia benki yetu kuwa kitovu cha huduma za kifedha kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati nchini.
“Tangu benki ifunguliwe mwaka 1995, benki imekuwa
haraka hali ambayo imesababisha mali za kampuni kufikia shilingi bilioni
190 mwishoni mwa mwaka 2011,” alisema Singili.
Singili aliongeza kuwa benki yake imelenga zaidi
katika kutoa huduma za kibenki za kipekee kwa bei nafuu ukiilinganisha
na mabenki mengine.
“Nawahakikishia kwamba tutaendelea kutoa
huduma za kipekee zinazokidhi mahitaji ya kila mteja wetu kwa upekee
wake. Katika miezi sita iliyopita benki imejikita katika mpango madhubuti
wa kujitanua kwa kufungua matawi matatu katika maeneo ya Mwenge jijini
Dar es Salaam, Arusha mjini katika barabara ya Wapare na mtaa wa sokoni
jijini Moshi,” alisema.
"Ninawaomba wateja wa benki ya Azania wa sasa na umma
kwa ujumla kuendelea kupata huduma mbalimbali za kibenki na huduma zinazotolewa
na benki hii ya Kitanzania yenye mafanikio," alisema.
Benki ya Azania iliaanzishwa mwaka 1995 kama
Adili Bancorp Limited baada ya Serikali kuruhusu mfumo wa uchumi wa
soko huria na kwa sasa benki hiyo ina wanahisa wakuu wakiwa pamoja
na mashirika ya serikali yakiwemo, National Social Security Fund (NSSF)
34.8%, Parastatal Pensions Fund (PPF) 30.1%, Public Service Pensions
Fund (PSPF) 17.2%, Local Authorities Pensions Fund (LAPF) 14.2%, na
mengine.
JANUARI MAKAMBA AITAKA TCRA KUTATUA KERO ZA MAWASILIANO YA MITANDAO HARAKA
Naibu
waziri wa Nishati na Madini January Makamba akiongea na waandishi wa
habari leo hii katika makao makuu ya mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
(TCRA) wakati wa ziara yake katika makao makuu hayo, ambapo aliipa TCRA
wiki mbili kufuatilia na kujadili na kutoa taarifa juu ya kero za
mawasiliano kwenye mitandao ya simu ikiwemo kukatika kwa network, pamoja
na huduma za kuhifadhia pesa katika simu.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria katika ziara hiyo ya January Makamba.
Tigo waanzisha promosheni ya Xtreme Pack
Meneja wa Huduma za malipo ya kabla Tigo Bw, Suleiman Bushagama
akizungumza na waandishi wa habari leo hii makao makuu ya Tigo jijini
Dar es Salaam, katika uzinduzi wa promosheni mpya ya iitwayo Xtreme Pack
ambapo mteja wa tigo anaweza kutuma meseji mbili za kulipia na kupata
meseji tano za bure kwenda mitandao yote nchini.
Kwakupiga
*148*01# au
kutumaneno XTREME kwenda namba 15509, wateja wa huduma yakulipia kabla
watafurahia huduma za thamani ambazo ni pamoja na dakika
15 za muda wa maongezi zitakazowawezesha kupiga simu Tigo kwa Tigo, sms
100, 50 MB
kwa ajili ya kuperuzi facebook, kutumia mtandao, E-mail pamoja na
Twitter,vyote hivyo kwagharama ya Tsh 450
nakuokoa sh 4,600! Pia tigo itatuma ujumbe mfupi wa maneno bure kwa
wateja wao, kuwataarifu juu ya ukomo wa matumizi ya vifurushi vyao na
kuwaruhusu kujiunga tena kama watahitaji.
Promosheni hiyo inaanza
kutumika rasmi kesho kushoto ni Titus Kafuma meneja wa Tigo internet na
kulia ni Alice Maro Msemaji wa Tigo, Naye afisa mahusiano wa Tigo Bi
Alice Maro alisema kuwa wanatafuta njia thabiti ya kuhakikisha kuwa
wateja wao wanapata huduma zinazoendana na thamani ya pesa zao.
Mmoja
wa waandishi wa habari Omary Katanga kutoka Redio one akiuliza swali
kwenye mkutano huo pamoja na waandishi wa habari wengine wanaoonekana
nyuma yake.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria kwenye uzinduzi huo wa Xtreme Pack ya Tigo.
Kamati ya PAC kutembelea waathirika wa Mabomu Mbagala Kuu
Wajumbe wa kamati ya PAC wakiwa kwenye mkutano wa utoaji taarifa ya maafa ya Mabomu Mbagala chini ya Mwenyekiti John Cheyo
Wakiangalia orodha ya malipo ya waathirika wa mabomu ya Mbagala
Muathirika Mzee Steven Gimongi (shoto)
akitoa maelezo alivyoathirika wakati wa mabomu mbele ya Mk wa Kamati ya (
PAC )John Cheyo
Mwenyekiti wa( PAC) John Cheyo (koti)
,MP wa Kigamboni Dk. Faustin Ndugulile (kaunda) pamoja na baadhi ya
wajumbe wa PAC na watenda
Mbunge wa Kigamboni Dr. Faustin Ndugulile (kaunda suti) akiwasikiliza baadhi ya waathirika wa mabomu huko Mbagala Kuu.
Rais Kikwete aongoza mafunzo ya Wakuu wa Mikoa na Wilaya mjini Dodoma
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri mkuu Mizengo
Pinda na Wziri wa TAMISEMI Hawa Ghasia wakiongoza Mafunzo ya Wakuu wa mikoa,
Makatibu Tawala wa mikoa na Wakuu wa wilaya yanayofanyika katika ukumbi wa
St.Gaspar mkoani Dodoma.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza wakati
mafunzo ya wakuu wa mikoa,makatibu tawala na wakuu wa wilaya inayoendelea
katika ukumbi wa St.Gaspar mkoani Dodoma.
Baadhi ya Wakuu wa Mikoa na wilaya wanaoshiriki
katika mafunzo katika ukumbi wa St.Gaspar mkoani Dodoma(picha na Freddy Maro)
Mkutano kundi la G77 and China katika mkutano wa mazingira jijini Bonn
Bi Fauzia Mwita, kutoka Idara ya Mazingira Zanzibar, akishiriki katika
majadililiano ya kuweka msimamo wa pamoja wa nchi zinazoendele katika
mkutano wa kundi la G77 and China, katika mkutano wa mabadiliko ya Tabia
nchi unaoendelea mjini Bonn.
Mkurugenzi wa mzingira zanzibar Bw Sheha Mjaja, akifuatilia mjadala wa
kuweka msimamo wa pamoja wa nchi zinazoendelea katika mkutano wa kundi
la G77 na China, kwenye Mkutano wa mabadiliko ya Tabia nchi unaendelea
mjini Bonn
Bw. Ladsalus Kyaruzi, na Injinia Alphonce Bikulamchi Maafisa
Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais wakishiriki katika majadiliano
ya kuweka msimamo wa pamoja wa nchi zinazoendelea katika kundi la G77 na
China.katika mkutano wa mabadiliko ya tabia nchi unaoendelea mjini
Bonn. (Picha na Evelyn Mkokoi)
Redds Miss Chan'gombe hiyooo yaja!!
Mashindano
ya kuwania taji la Redds Miss Tanzania 2012 yanazidi kupamba moto kwa
ngazi za vitongoji nchini kote huku vitongoji kadhaa vikiwa tayari
vimesha fanya mashindano yake na vingine vikiendelea na maandalizi.
Wakati
wiki hii Mashindano hayo yakitraji kufanyika katika Vitongoji vya
Kurasini Jijini Dar es Salaam tayari Wanyange wanaowania taji la Redds
Miss Cha'gombe 2012 nao wapo katika mazoezi tayari kwa fainali zao
zitakazo fanyika mapema mwezi ujao.
Pichani
ni warembo wa Chan'gombe wakiwa katika picha ya pamoja iliyopigwa muda
mfupi baada ya kumaliza mazoezi yao Mei 22,2012 katika ukumbi wa TCC
Chan'gombe jijini Dar es Salaam.
Warembo hao 11 wanataraji kupanda jukwaani mapema mwezi ujao kuwania taji hilo na kuwania tiketi ya kushiriki Miss Temeke 2012.
Waziri Amos Makala akutana na wananchi kujadili mgogoro wa Ardhi Kinyenze
Mbunge
wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla ( aliyesimama na kunyosha mkono juu)
akisisitiza jambo juu ya namna ya kutafuta muakafa ili kumalizwa
kwa mgogoro wa ardhi kati ya wananchi wa Kitongoji cha Kinyenzi dhidi
ya Mwekezaji wa kizungu.
Mzee Said Ahamad Kondo ( aliyesimama) akiuliza maswali kwenye mkutano
wa hadhara ulioitishwa na Mbunge wa Jimbo la Mvomero , Amos Makalla (
hayupo pichani) alipokuwa katika Kitongoji cha Kinyenze, Kijiji cha
Kipera, Tarafa ya Mlali kufuatilia mgogoro kati ya Wananchi hao na
Mwekezaji wa Kizungu.
Ofisa Ardhi wa Wilaya ya Mvomero, Majaliwa Jafari ( aliyesimama) akitoa ufafanuzi wa mgogoro wa shamba namba shamba 296 kati ya wanachi wa Kitongoji cha Kinyenze na Mwekezaji wa Kizungu kwenye mkutano
wa Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla, ambaye pia ni Naibu Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo , uliofanyika hivi karibini (
Mei 19) uliokuwa na lengo la kufikia utatuzi wa mgogoro huo
Baadhi
ya wazee na wananchi wa Kitogoji cha Kinyenze, Kijiji cha Kipera,Tarafa
ya Mlali, Wilaya ya Mvomero, wakimsikiliza kwa makini Mbunge wa Jimbo
hilo, Amos Makalla ( hayupo pichani) wakati akipowatembelea hivi
karibuni ( Mei 19) wananchi wa Kitongoji hicho kwa ajili ya kupanga
mkakati wa kumalizwa
mgogoro kati ya mwekezaji wa kizungu na wakazi hao, Mbunge huyo pia ni
Naibu Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo.
Subscribe to:
Posts (Atom)