- CHADEMA ni chama cha itikadi ya MRENGO WA KATI (center party).
- CHADEMA ni chama kinachoamini kukuza na kuimarisha uchumi wa
nchi kwa kutumia raslimali za nchi yetu bila kuathiri uhuru wa Taifa, na
kuhakikisha kuwa umma kwa ujumla unanufaika na raslimali zao.
- CHADEMA inaamini katika kujenga na kuimarisha uchumi wa soko
huru, utakaoheshimu na kulinda haki na mali za watu, biashara huru na
sekta ya watu binafsi bila kupoka mamlaka ya umma katika maeneo nyeti
hususani pale penye hitilafu ya soko au penye maeneo nyeti ya kiuchumi.
Tunaamini katika soko huru sio soko holela.
- CHADEMA inaamini kuhakikisha matumizi bora ya raslimali asilia
za nchi ili zichangie kikamilifu katika pato la taifa na hasa kuboresha
huduma za kiuchumi zinazotumiwa na wananchi wote.
- CHADEMA inaamini katika uzalendo na kuthamini mila na desturi zetu zilizo nzuri.
- CHADEMA inaamini katika uhuru chini ya sheria zilizo za haki.
- CHADEMA inaamini katika siasa ambazo ziko juu ya vyama zenye kusimamia zaidi maslahi ya Taifa.
- CHADEMA inaweka umuhimu wa pekee katika familia kama moja ya taasisi muhimu ya kijamii.
- CHADEMA inaamini katika umuhimu wa uhuru wa kuamini katika
kujenga maadili ya mwanajamii mmoja mmoja bila kuifanya dini kuwa sehemu
ya dola.
- CHADEMA inaamini taifa linaundwa na watu, hivyo uhai wake unawategemea watu, na mabadiliko yake yanatokana na watu.
- CHADEMA inaamini katika kujenga uwezo wa wazawa katika kumiliki na kuendesha uchumi.
- CHADEMA inaamini kumiliki raslimali na mali miongoni mwa wananchi kunawapa uhuru zaidi hivyo tunataka kujenga chama na baadaye taifa lenye kutoa fursa, ambapo kila mtu bila kujali asili na hali yake anaweza kutimiza na kufanikiwa kadiri ya vipaji vyake.
Tuesday, May 1, 2012
Itikadi ya Chama
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment