Mwanasheria Thomas Fortune Fay wa Kampuni ya sheria ya Fay Kaplan
iliyoko Washington DCMarekani.
ZAIDI ya miaka kumi
na tatu baada ya milipuko ya mabomu ya kujitoa mhanga iliyotokea kwenye Ubalozi
wa Marekani jijini Dar es Salam Agosti
7,1998, mmoja wa ndugu wa marehemu amemtaka Jim Owen kutoa taarifa kuwa ni lini
fidia itaanza kulipwa.
Kauli hiyo
ilitolewa jijini Dar es Salaam leo, Kulwa Mbogo ambaye pacha wake aliyekuwa
akifanya kazi katika ubalozi huo alifariki katika tukio hilo.
Alisema walipata
taarifa kuwa mmoja wa majeruhi,
Owen ambaye ni raia wa Marekani huku akiwa ameoa Mtanzania alifungua kesi
ya madai ya fidia kuhusu
Watanzania zaidi ya kumi ambapo kesi hiyo imekamilika hivi karibuni.
Mbogo alisema kupitia
vyombo vya habari waliambiwa kuwa mchakato wa malipo ya fidia hiyo utakuwa
umekamilika hadi kufikia mwishoni mwa Mei mwaka huu lakini hadi leo hakuna hawajapatiwa
nyaraka zozote zinazoonyesha kuwa wataanza kulipwa lini na kwa sitaili gani.
“Shauli hilo alimkabidhi
mwanasheria wake Thomas Fortune Fay na Kampuni yake ya sheria ya Fay Kaplan
iliyoko Washington DC ambayo iliwaunganisha raia wa Tanzania katika kesi hiyo
ambapo walifanya mawasiliano na waathirika wa tukio hilo mara kwa mara”alisema
Mbogo.
Mbogo alisema yeye
ni miongoni mwa familia ya
waathirika na mabomu hayo ambapo walijiorodhesha katika kesi hiyo iliyokuwa
ikiendeshwa na mwanasheria huyo.
Naye Owen ambaye ni
mwakilishi wa msimamizi wa malipo hayo hapa nchini kupitia, Fuadi Latifu
alisema malipo hayo yataanza kulipwa kuanzia Julai mwaka huu baada ya
kukamilika mchakato mzima wa maandalizi ya malipo hayo ikiwa ni kufunguliwa
Akaunti za Benki kwa kila mhusika.
Fuad
Latif alisema ni mara ya kwanza na historia kwa nchi hiyo kutoa haki hiyo kwa
watu kutoka taifa jingine ambapo haki hiyo imekuja baada ya Kampuni hiyo ya
Sheria kuwapigania Watanzania hao.
No comments:
Post a Comment