Posted: 11 May 2012 01:14 AM PDT
Wawekezaji wa madini wamponza mchimbaji
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Bw.Diwani Athuman, alisema Bw.
Magunila, alishambuliwa juzi mchana na kundi la wachimbaji wadogo wadogo
katika machimbo ya dhahabu yaliyopo kijiji cha Mhandu kata ya Chela,
wilayani Kahama.
Bw.Athuman
alisema siku ya tukio hilo, Bw.Magunila alikuwa amefuatana na
wawekezaji kutoka nje ya nchi na kwenda nao katika machimbo hayo bila
kuwashirikisha, kitu walichomtuhumu anataka kuuza eneo hilo kwa maslahi
yake binafsi, ndipo walipoanza kumshambulia kwa mawe na marungu.
Akiongea
kwa taabu na mwandishi wa habari hizi alikolazwa katika Hospitali ya
Wilaya ya Kahama, Bw. Magunila, alisema eneo hilo ni mali yao na Mkuu wa
Wilaya Meja Matala kwa vile wameshalikatia leseni kutoka mwaka jana.
Bw.Magunila
alisema eneo la machimbo ya dhahabu la Mhandu walishalikatia leseni ya
majina mawili yeye na Meja Matala, ambapo wana viwanja sita.
Wachimbaji
wadogo wadogo katika eneo hilo ambao hawakupenda majina yao yaandikwe
gazetini waliwatuhumu Meja Matala na Magunila kutumia ujanja wa
kulichukua eneo hilo bila wao kuwashirikisha.
Diwani wa Kata ya
Chela Bw. Mibako Mabubu, alisema Bw.Magunila, alifanya kosa kwenda eneo
hilo bila kushirikisha viongozi wa kata pamoja na kudai ana leseni ya
viwanja sita.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Meja Matala alipoulizwa
alikiri kuwepo kwa tukio hilo ila akasema hawezi akalizungumzia suala
hilo kama Bw.Magunila.
Ofisa Madini Mkazi wa Wilaya ya Kahama
Bw.Tuna Badoma, alipotakiwa kuthibitisha kuhusu leseni ya Bw.Magunila na
Meja Matala alisema yeye si msemaji
|
Posted: 11 May 2012 01:07 AM PDT
Na Godfrey Ismaely, Dar es Salaam
IMEBAINISHWA
kuwa demokrasia iliyopo Tanzania ni moja wapo ya chachu inayowafanya
watu wengi zikiwemo nchi zilizoendelea duniani kutamani kuwa nayo,
lakini inashindikana kutokana na mifumo yao ya kiutawala.
Mbali
na hayo Watanzania wamehimizwa kuendelea kuilinda, kuheshimu na kuitumia
vyema demokrasia hiyo katika kujadili ikiwemo kuibua mambo ambayo
hayana uchochezi ili kuharakisha maendeleo yao.
Changamoto
hiyo ilitolewa juzi na Waziri Mkuu mstaafu wa Rwanda Bw. Faustine
Twagiramungu ambaye kwa sasa anaishi mjini Brussels nchini Ubeligiji
wakati akichangia mada kwenye kipindi cha Straight Talk Afrika ambacho
huwa kinarushwa na Sauti ya Amerika (VOA) kutoka mjini Washington DC
nchini Marekani.
Hata hivyo sababu kuu iliyomsukuma Waziri huyo
mstaafu kutamka hivyo ni kutokana na mada ambayo iliwasilishwa katika
kipindi hicho ambayo iliangazia tija ambayo inaweza kupatikana kwa Bara
la Afrika baada ya Wafaransa kufanya uamuzi wa kidemokrasia na
kumuingiza madarakani Bw. Francois Hollande.
"Huwezi kumpima mtu
kwa matendo yake ila uamuzi na siasa safi hususan demokrasia zenye
mantiki kwa Afrika ndizo kimbilio na ufunguo wa maendeleo kwa Afrika;
"Nikiwa
huku nilipo (Ubeligiji) nchi ambazo ninaweza kujivunia kuwa na
demokrasia ya kweli si kwetu Rwanda... ni Tanzania na ninaamini iwapo
wataitukuza (Watanzania) demokrasia hiyo ni fundisho pekee na mfano wa
kuigwa katika Bara la Afrika na hata nje ya bara letu," alisema Bw.
Twagiramungu.
Hata hivyo baadhi ya wachangiaji wa mada hiyo
kutoka sehemu mbalimbali duniani walisema kuwa, nchi za Afrika ikiwemo
Tanzania haziwezi kutegemea wahisani kuziendesha ila umefika wakati sasa
rasilimali zinazowazunguka kutumika vyema kwa manufaa ya Waafrika.
"Kuchaguliwa
kwa Rais mpya nchini Ufarasa kwetu (Afrika) si tija, haijalishi sera
zake zinajikita katika Ujamaa au la!...tutakachofanya ni kuendelea
kudumisha umoja na ushirikiano, lakini masuala ya uwajibikaji kwa
manufaa ya nchi zetu yanatuhusu wenyewe," alisema mmoja wa wachangiaji
wa mada hiyo kutoka nchini Nigeria.
Hata hivyo tafiti zinaonesha
kuwa mbali na changamoto za hapa na pale demokrasia iliyopo Tanzania
imekuwa mfano wa kuigwa kutokana na Watanzania wenyewe kuwa na maamuzi
yao pekee bila kulazimishwa na watu ya kuwachagua ikiwemo kuwakataa
viongozi ambao wanaona hawawajibiki ipasavyo.
|
Posted: 11 May 2012 01:01 AM PDT
|
Posted: 11 May 2012 12:59 AM PDT
Na Jovin Mihambi, Mwanza
MKUU
wa Mkoa wa Mwanza, Bw. Evarist Ndikillo, amewataka wafanyabiashara
nchini kuagiza bidhaa kutoka nchi za nje zenye ubora unaokidhi viwango
vya kimataifa na vinavyoendana na uchumi wa nchi ili kila mwananchi
aweze kumudu kuvinunua na vitumike kwa muda mrefu.
Hayo
yalisemwa na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Bw. Saidi Amanzi, katika
hotuba yake aliyoitoa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, wakati wa
ufunguzi wa duka la kuuza pikipiki na bidhaa zingine zinazotengenezwa na
kampuni ya Honda ambalo limefunguliwa na Kampuni ya QM Quality Motors
Limited lenye makao makuu yake jijini Dar es Salaam.
Alisema kuwa baadhi ya wafanyabiashara nchini wamekuwa wakiingiza bidhaa mbalimbali ambazo hazina ubora na nyingi kutoka China.
Alisema
kufunguliwa kwa duka hilo la kuuza pikipiki za Honda pamoja na bidhaa
zingine ambazo ni jenereta, pampu za kusukumia maji, injini za
kuendeshea mitumbwi limekuwa ni mkombozi kwa wananchi wa kanda ya Ziwa
na mikoa mingine ya jirani.
Naye Meneja mauzo na Masoko wa
kampuni ya QM Quality Motors Limited, Bw.Sudhir Borgaonkar, alisema
bidhaa za kampuni yake ikiwemo pikipiki za Honda ambazo alisema zinauzwa
bei nafuu ikilinganishwa na zile za kutoka China.
|
Posted: 11 May 2012 12:58 AM PDT
Diwani
wa Kata Vijibweni Bw.Selemani Methew akimpa pole mzazi aliyejifungua
watoto mapacha Bi.Robi Wambura katika Hospitali ya Vijibweni Wilaya
Temeke, Dar es Salaam juzi, (Picha na Heri Shaaban)
|
Posted: 11 May 2012 12:52 AM PDT
Na Mwali Ibrahim
KOCHA
Mkuu wa timu ya Taifa ya Wanawake ya Zimbabwe Rosemary Mugdza amesema
kikosi chake kipo kamili kukabiliana na timu ya Taifa ya wanawake 'Twiga
Star' katika mchezo wake wa kirafiki wa kimataifa utakaochezwa kesho
katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Akizungumza
Dar es Salaam jana, kocha huyo alisema, walikuwa wakisaka timu ya
kucheza nayo ikiwa ni kwa ajili ya maandalizi yao na mechi ya Nigeria
ambapo waliamua kuichagua Tanzania kutokana na uwezo mkubwa waliokuwa
nao.
"Twiga ni timu nzuri na yenye uwezo na ndio maana tuliona ni
timu ya kuchuana nayo tukiwa katika maandalizi ya mchezo wetu huo kwani
tunaimani tutapata mazoezi ya kutosha," alisema.
Aliongeza kuwa
kwa upande wa maandalizi wamejiandaa vya kutosha hivyo wanaimani kubwa
ya kufanya vizuri katika mchezo huo ili kujiweka katika nafasi nzuri
katika mchezo wao ujao.
Kwa upande wake Ofisa Habari wa
Shirikisho la soka nchini (TFF) Bonifance Wambura akizungumza kwa niaba
ya kocha wa Twiga, Boniface Mkwasa alisema hata kwa upande wao mchezo
huo utakuwa ni mchezo mmoja wa kimataifa ambao ni kwa ajili ya mechi ya
maandalizi ya kuivaa Ethiopia Mei 26, mjini Adis Ababa.
"Huu ni
mchezo wa kwanza wa kimataifa wa kirafiki kwa ajili ya kujiweka sawa
kwani timu hii itacheza mchezo mwingine wa kirafiki Mei 20 ambapo kwa
sasa tunatafuta timu ya kucheza nayo," alisema.
Alisema, timu
hiyo ilikuwa mkoani Mwanza ikimalizia ziara yake ya kucheza michezo
mbalimbali ya kujipima nguvu ambapo sambamba na mkoa huo pia walicheza
mchezo mmoja mkoani Dodoma.
Wambura alisema, kwa upande wao wako
tayari kukabiliana na timu hiyo kwani wanaijua vizuri walishawahi
kuchuana nayo katika mashindano ya All African Games mwaka jana.
Alitaja
viingilio katika mchezo huo kuwa VIP A ni sh. 10,000, VIP B sh. 5,000
na viti vingine vikiwa ni sh. 1,000 ambapo wanaimani mashabiki
watajitokeza kwa wingi kuisapoti timu hiyo..
|
Posted: 11 May 2012 12:47 AM PDT
Na Stella Aron
WANANCHI
wametakiwa kujitokeza kwa wingi kupima afya zao bure ili kuzuia na
kutibu magonjwa mbalimbali yanayoangamiza jamii kwa asilimia kubwa.
Hayo
yalisemwa jana Dar es Salaam na Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Agakhan
Bi. Loveluck Mwasha, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu
maandalizi ya siku ya uuguzi duniani, ambayo huadhimishwa Mei 12, kila
mwaka.
Alisema katika
kusherehekea siku hiyo uongozi wa hospitali hiyo umeazimia kutoa huduma
ya upimaji bure kwa magonjwa ya kisukari na shinikizo la damu kesho
katika ukumbi wa Mlimani City.
"Tumechagua magonjwa hayo kutokana
na watu wengi kupoteza maisha kwa kutofahamu dalili za magonjwa hayo
kwa kushindwa kupata huduma za matibabu, " alisema Bi.Mwasha.
Bi.Mwasha
alisema siku hiyo watatoa ushauri mbalimbali kwa watu warefu au wafupi
na wenye uzito mkubwa namna ya kupunguza uzito ili kuepukana na ugonjwa
wa shinikizo la damu na magonjwa mengine nyemelezi.
Alisema
wananchi watakaogundulika kuwa na magonjwa hayo watatakiwa kwenda kwenye
vituo vya afya kwa ajili ya kupata huduma zaidi, ambapo hivi sasa kuna
idadi kubwa ya watu wanaougua magonjwa hayo lakini hawajitambui.
"Kwa
wastani wa mwezi Agakhan tunapokea wagonjwa 50 wa kisukari ambao hupata
tiba na kurejea majumbani mbali ya wale wanaolazwa," alisema Bi.
Mwasha.
Muuguzi huyo alisema kabla ya kusherehekea siku hiyo
uongozi wa hospitali hiyo jana ulitoa mafunzo kwa wauguzi wake namna ya
kufuata maadili ya kazi na utoaji wa chanjo.
"Tumetoa mafunzo kwa
wauguzi wetu ili waweze kukumbuka na kufuata maadili ya kazi zao na
utoaji wa ushauri kwa jamii kufahamu umuhimu wa chanjo, " alisema.
|
Posted: 11 May 2012 12:46 AM PDT
Diwani
wa kata ya kilosa wiliya ya Nyasa Bw. Issa Mustapha (kulia) akimuekeza
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Bw.Said Mwambungu (wa tatu kulia) nama
ilivyonusurika kuuawa na wananchi wa kata hiyo baada ya kuwakatalia
kushiriki kuongoza zoezi la kutoa uchawi kwa watu waliotuhumiwa kuhusika
na vitendo vya kishirikina katika eneo hilo, wengine ni wajumbe wa
kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huo.Picha na kassian Nyandindi
|
Posted: 11 May 2012 12:31 AM PDT
Na Rehema Mohamed
MAHAKAMA
ya Hakimu Mkazi Kisutu imeshindwa kuendelea kusikiliza kesi ya
kupatikana na simu gerezani inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa
Utumishi na Utawala wa Benki Kuu (BoT), Bw. Amatus Liyumba, kutokana na
hakimu anayesikiliza kesi hiyo kutokuwepo mahakamani.
Wakili wa
Serikali Bi.Elizabert Kaganda, alisema jana mbele ya hakimu Bi.Devota
Kisoka, wakati kesi hiyo ilipotajwa mahakamani hapo. Alisema Bw.Suwart
Sanga anaumwa hivyo ameshindwa kufika mahakamani.
Kutokana na
hali hiyo kesi hiyo imepangwa kuendelea kusikilizwa Julai 2, mwaka huu.
Katika kesi hiyo inadaiwa kuwa, Julai 27, mwaka jana, Bw.Liyumba akiwa
mfungwa kwenye gereza la Ukonga anadaiwa kukutwa na kifaa kilichozuiliwa
kisheria ambacho ni simu aina ya Nokia, rangi nyeusi yenye laini namba
0653004662 na IMEI 356273/04/276170/3.
|
Posted: 11 May 2012 12:29 AM PDT
|
Posted: 11 May 2012 12:27 AM PDT
Na Elizabeth Mayemba
KAMPUNI
ya Simu za mikononi ya Airtel jana ilizindua awamu ya pili ya mpango
kabambe wa mpira wa miguu nchini Airtel Rising, ambao nia yake ni
kutafuta na kukuza vipaji vya mchezo huo kutoka ngazi ya chini kabisa
mpaka ya taifa.
Michuano ya
Airtel Rising Stars iliyozinduliwa na mchezaji wa zamani wa Manchester
United Quinton Fortune, itaanza kutimua vumbi Mei 24 mwaka huu, kutoka
mikoa sita, fomu za usajili zinapatikana kwenye makao makuu ya ofisi za
Airtel Lindi,Mbeya,Arusha,Kinondoni, Ilala na Temeke.
Awamu ya
kwanza ya mpango huu ilifanyika mwaka jana na kupata mafanikio makubwa,
lengo likiwa ni kuvipika vipaji vinavyochipukia chini ya umri wa miaka
17, nafasi ya kuonyesha vipaji vyao kwa makocha waliobobea pia kupata
nafasi ya kuendeleza vipaji vyao.
Akizungumza Dar es Salaam jana
kwenye uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania Sam
Elangallor alisema, mafanikio ya mwaka jana yanaonesha mpira wa miguu
una uwezo wa kuunganisha makabila mbalimbali na pia kuleta hamasa kwa
jamii ya chini hadi taifa.
"Mwaka jana zaidi ya timu 11,000
Afrika zilijiandikisha kushiriki kwenye michuano hii kuanzia kwenye
mtoano na kuchagua wachezaji ambao waliunda timu zilizoshiriki kwenye
ngazi ya mkoa, ushiriki huu mkubwa ulituonesha ya kwamba tuko kwenye
njia sahihi, na ndio maana tuna hamasa kubwa na awamu hii ya pili kwa
mwaka huu," alisema Elangallor
Alisema kama ilivyokuwa kwa mwaka
jana, mpango huu utaanzia ngazi ya mkoa na taifa na kufuatiwa na kliniki
ya soka ya kimataifa chini ya wakufunzi kutoka klabu ya Manchester
United ya Uingereza, kwa mwaka huu kutakuwa na mashindano ya siku nne ya
timu bingwa kutoka kila nchi itakayoshiriki kushindania taji jipya la
Airtel Rising Stars African Champion.
Kwa mwaka huu michuano hii
imezinduliwa na mchezaji wa zamani wa Manchester United Quinton Fortune,
mchezaji aliyesajiliwa na kocha Sir Alex Ferguson mwaka 1999 akitokea
klabu ya Atletico Madrid wakati huo akiisaidia timu yake kushinda
vikombe vitatu.
Raia huyo wa Afrika kusini aliweza kuzoea haraka
mazingira wa Uingereza na kuweza kupata namba ya kudumu kwenye kikosi
cha Ferguson kama winga wa kulia,kiungo wa kati na mshambuliaji, akiwa
Man U Fortune aliiwezesha timu yake kushinda taji la FA mwaka 2003.
|
Posted: 11 May 2012 12:25 AM PDT
Mchezaji
wa zamani wa Klabu ya Manchester United ya Uingereza Quinton Fortune,
akipiga mpira kuashiria uzinduzi rasmi wa michuano ya vijana wenye umri
chini ya miaka 17 ya Airtel Rising Stars. Uzinduzi huo ulifanyika jana,
kwenye Hoteli ya Sea Clif, jijini Dar es Salaam.(Na Mpigapicha Wetu)
|
Posted: 11 May 2012 12:22 AM PDT
Na Heri Shaaban
UONGOZI
wa Kata Vijibweni iliyopo Kigamboni wamemuagiza Mganga Mkuu Zahanati ya
Vijibweni, Bi.Rukia Msumi, kuagiza walinzi wa zahanati hiyo kuacha geti
wazi ili wagonjwa waweze kuingia baada ya kutokea tukio la mjamzito
kujifungulia getini.
Agizo hilo
lilitolewa juzi wakati wa ziara ya kushtukiza iliyofanywa na diwani
huyo, Bw. Suleiman Methew akiongozana na wenyeviti wake. Alikemea vikali
kitendo cha walinzi kukataa kufungua milango hadi mjamzito
akajifungulia nje.
Bw. Methew alimtaka mganga mkuu awaagize walinzi wa hospitali hiyo kuruhusu magari kuingia ndani wakati wote.
Bw.Methew
alisema baada ya kupata malalamiko ya makosa yanayofanywa na walinzi
wa zahanati hiyo kwa muda mrefu yeye kama kiongozi amekerwa.
"Wananchi
wangu kufanyiwa vitendo vya aina hii sijaridhika navyo, kuanzia leo
naomba magari yote ya wagonjwa yaingie ndani kama vituo vingine vya afya
wanavyofanya pindi wanapopokea wagonjwa," alisema Bw.Methew.
Alimtaka mganga huyo kusimamia suala hilo ili vitendo vya aina hiyo visijirudie.
Kwa
upande wake Mganga Mkuu, Bi.Rukia Msumi, alisema taarifa hizo
zilimfikia na alitoa onyo lakini kampuni hiyo ya ulinzi ilipuuzia.
|
Posted: 11 May 2012 12:20 AM PDT
Askari
wa doria wakikagua pikipiki baada ya kuzikamata kwenye makutano ya
Barabara za Bibi Titi Mohamed na Uhuru, Dar es Salaam jana. (Picha na
Charles Lucas)
|
Posted: 11 May 2012 12:17 AM PDT
Na Queen Lema, Arusha
WAFANYAKAZI
wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Arusha wamedai afya zao zipo hatarini
kutokana na kukosa choo na kusababisha mazingira ya ofisi hiyo kutapakaa
maji machafu.
Suala hilo limekuwa likilalamikiwa kwa zaidi ya
mwaka mmoja bila kupatiwa ufumbuzi huku wafanyakazi hao wakiendelea
kukumbwa na adha ya harufu mbaya.
Wakizungumza
na waandishi wa habari kwa sharti la kutonukuliwa majina yao kwenye
vyombo vya habari, walisema adha hiyo imekuwa ikiwakumba zaidi watumishi
waliopo chini ya jengo hilo la ofisi ya mkuu wa wilaya.
Mmoja wa
watumishi hao alisema watumishi waliopo ghorofa ya juu wamekuwa
wakimwaga maji na kusababisha choo cha chini kuzagaa uchafu.
"Kama
mnavyoona hii hali inatisha kwani ni muda mrefu choo hiki kimeziba
wenzetu wakimwaga maji huko juu, uchafu wote unatoka," alisema mtumishi
huyo.
Wafanyakazi hao kutoka idara mbalimbali za serikali katika
jengo hilo, walidai kuwa wamekuwa wakipata shida kutokana na kukosa
sehemu ya kujisaidia na kulazimika kwenda umbali mrefu kutafuta huduma
hiyo ya choo.
Alidai taarifa ya ubovu wa choo hicho walitoa kwa
viongozi akiwemo aliyekuwa Mkuu wa Wilaya Bw.Raymond Mushi, bila
kupatiwa ufumbuzi. Kukosekana kwa huduma ya choo katika jengo hilo
kumewakumba watumishi wa idara mbalimbali za Serikali.
Akizungumzia
hali hiyo Katibu Tawala wa Wilaya, Bw. Emi Lyimo, alikiri kupata
taarifa juu ya ubovu wa choo hicho, lakini alidai kuwa suala hilo lipo
juu yake na tayari taarifa walishazifikisha ofisi kunakohusika.
Alisema hali ya ubovu wa choo hicho ni ya siku nyingi hata Mkuu wa Wilaya anaifahamu.
Kwa
upande wa Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Bw. Everin Itanisa, alipoulizwa
kuhusu ubovu wa choo katika jengo hilo alidai kuwa taarifa hizo anazo
na kilichokwamisha ukarabati ni ukosefu wa fedha.
Alisema
ukarabati wa choo hicho unahitaji gharama kiasi cha sh.milioni 12 na
ofisi yake haikuwa na fedha isipokuwa wamepata nusu baada ya kuamua
kuchangishana katika idara zote za ofisi.
|
Posted: 11 May 2012 12:14 AM PDT
Mkurugenzi
wa Taasisi ya Tanzania Homes Expo, inayojishughulisha na makazi, Bw.
Zenno Ngowi, akisoma taarifa kwa waandishi wa habari (hawapo pichani),
Dar es Salaam jana, kuhusu Maonesho ya Sekta ya Nyumba yatakayofanyika,
Dar es Salaam, mwezi juni, mwaka huu. kushoto ni Mratibu wa Matukio wa
taasisi hiyo Bw. Richard Mvula na Meneja Masoko Bi. Nice Chande. (Picha
na Charles Lucas)
|
Posted: 11 May 2012 12:10 AM PDT
Darlin Said na Radhia Adam
KAMPUNI
ya Mobile Ticketing LTD imezindua huduma mpya ya kukata tiketi za
usafiri wa mabasi yaendayo mikoani na nchi za jirani inayojulikana kwa
jina la "Tiketi popote" kwa kutumia simu za mikononi ambapo mteja
atapata huduma ya tiketi popote alipo.
Huduma
hiyo inategemewa kutumika kwa mikoa yote ya Tanzania ambapo kwa sasa
huduma hiyo itaanza kutolewa katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza,
Arusha, Tabora, Mtwara, Kilimanjaro, Lindi, Morogoro pamoja na nchi za
jirani.
Huduma hiyo imeanza kutumika rasmi mara baada ya
kuzinduliwa na kwa sasa inahusisha huduma za M-pesa, Airtel money pamoja
na Easypesa.
Akiongea na waandishi wa habari jana jijini Dar es
Salaam Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Bw.Abert Muchuruza, alisema
wameanzisha kampuni hiyo kwa lengo la kuondoa usumbufu wanaoupata
wasafiri pindi wanapoenda kukata tiketi ikiwemo kuuziwa tiketi bandia,
kuzidishiwa nauli na wapiga debe na kuuziwa tiketi za magari yasiyo
safiri.
Huduma hiyo inatoa taarifa zote za mteja ikiwemo namba ya
gari, namba ya siti pamoja na jina la gari atakalosafiri nalo abiria na
ikitokea tatizo, msafiri anajulishwa.
Mbali na huduma ya tiketi kwa mabasi kampuni inatarajia kutoa huduma kwa vyombo vingine vya usafiri kama treni na meli.
|
Posted: 11 May 2012 12:08 AM PDT
Askari
wa usalama Barabarani, akimuamuru dereva wa daladala namba T 225 BRD,
kuegesha gari hilo kando ya barabara ya Azikiwe, Posta Dar es Salaam
jana, baada ya kukiuka kanuni za usalama barabarani. (Picha na Charles
Lucas)
|
Posted: 11 May 2012 12:04 AM PDT
Na Elizabeth Mayemmba
TIMU
ya soka ya Simba imewasili salama jijini Khartoum, Sudan, jana usiku
majira ya saa 5:49 ikitokea jijini Nairobi, nchini Kenya tayari kwa
pambano lake la Kombe la Shirikisho (CAF) dhidi ya Al Ahly Shendi,
ambapo walipokelewa na uongozi wa Chama cha Soka cha Sudan (SFA) lakini
Hata
hivyo timu hiyo ilikiona cha moto kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
wa Khartoumbaada baada ya kutua kwa kuwekwa uwanjani hapo kuanzia saa
sita usiku hadi saa saba na nusu usiku kwa kisingizio cha kumalizia
taratibu za kiulinzi na kiusalama uwanjani hapo.
Kiongozi wa SFA
alipoulizwa kwanini wachezaji wanazidi kuwekwa uwanjani hapo wakati ni
usiku wa manane , kiongozi huyo alijibu kwa mkato kuwa"Hata kwenu pia
mlifanya hivihivi.”
Simba walitakiwa kuingia Sudan saa mbili
usiku lakini walichelewa kufika kutokana na hitilafu iliyokuwepo katika
ndege ya Shirika la Ndege la Kenya (Kenya Airways) iliyopaswa iwachukue
kutoka Nairobi.
Msafara huo wa Simba wa wachezaji 19 na viongozi
wanane ulifikia katika Hoteli ya Shariqa lakini jana timu hiyo ilitakiwa
kusafirishwa kwenda katika mji wa Shendi uliopo umbali wa Kilomita 150
kutoka Khartoum. Mechi ya Shendi na Simba itapigwa Jumapili saa mbili
usiku katika Uwanja wa Shendi wenye uwezo wa kuchukua washabiki 10,000.
Kocha
Mkuu wa Simba, Profesa Milovan Cirkovic alisema jana asubuhi kikosi
chake hakikufanya mazoezi ya aina yoyote lakini jioni walifanya kama
kawaida.
"Kuna uwezekano mkubwa wa mazoezi ya leo (jana)
yakafanyika usiku muda ambao timu tutacheza ili wachezaji wazoee hali
hiyo," alisema Milovan
Timu zote mbili, Simba na Shendi zinaweza
kucheza kwa mara ya kwanza katika hatua ya makundi ya michuano ya Kombe
la CAF. Simba iliweza kufika fainali ya michuano hii mwaka 1992 lakini
wakati huo mfumo wa sasa wa hatua ya makundi katika hatua ya nane bora
ulikuwa haujaanza kutumika.
|
Posted: 11 May 2012 12:02 AM PDT
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Robin Goetzsche (kulia) na
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) Leodgar Tenga
(kushoto) wakisalimiana baada ya kusaini mkataba wa kuiwezesha TBL kuwa
mdhamini mkuu wa Timu ya Taifa-Taifa Stars kwa miaka mitano ijayo
kupitia Bia yake ya Kilimanjaro Premium Lager. Katikati ni Meneja wa Bia
ya Kilimanjaro premium Lager, George Kavishe. (Na Mpigapicha Wetu)
|
Posted: 10 May 2012 11:59 PM PDT
Na Elizabeth Mayemba
KAMPUNI
ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Kilimanjaro imeingia mkataba
wa kuidhamini timu ya taifa, Taifa Stars kwa kipindi cha miaka mitano
wenye thamani ya sh.bilioni 23 ambazo zitatumika katika kuimarisha timu
hiyo ambayo inapeperusha bendera ya Taifa.
Uzinduzi
huo ulifanyika katika hoteli ya Kempinski, Dar es Salaam na kuhudhuriwa
na viongozi wote wakuu wa TFF, TBL na wadau mbalimbali.
Awali Stars tangu mwaka 2006 ilikuwa ikidhaminiwa na kampuni ya Serengeti (SBL).
Akizungumza
katika hafla hiyo ya kutiliana saini, Mkurugenzi Mtendaji wa TBL, Robin
Goetzsche alisema udhamini huo utafungua mwanga mpya katika medani ya
soka nchini Tanzania.
“Tunasaini mkataba wa miaka mitano wenye
thamani ya dola za Marekani milioni 10 sawa na sh.bilioni 23 za Tanzania
utalifikisha soka letu Katika Kilele cha Mafanikio na kutupa kila
sababu ya kujivunia kilicho chetuTuna matarajio makubwa sana na timu ya
taifa kwani tunaamini kuwa ina uwezo wa kufanya maajabu, na kama
nilivyosema awali, hili ni pambazuko la kuelekea mafanikio.
"Uwekezaji
wetu umelenga katika kuhakikisha kambi za mazoezi zinaimarishwa,
wachezaji watalala katika hoteli zenye ubora wa juu zenye zaidi ya ngazi
tatu zilizo na bwawa la kuogelea na vifaa vya mazoezi, vifaa
vinaboreshwa na pia vijana watapata fursa za kucheza mechi nyingi za
kirafiki ili wajipime nguvu na kupata uzoefu zaidi na timu zinapata basi
jipya la kisasa," alisema
Alisema udhamini wao utasaidia
katika ununuzi wa vifaa mbalimbali vya kisasa vya michezo, mafunzo kwa
wafanyakazi wa TFF ndani na nje ya nchi, uendeshaji wa tovuti ya TFF,
Semina na mikutano ya utawala bora.
Alisema wanaamini kabisa
juhudi madhubuti zikiwekwa kwa kushirikiana na TFF na wadau wengine,
malengo ya kuifanya Timu ya Taifa ishinde mechi zake zote yatatimia.
Goetzsche
alisema TFF peke yake au mdhamini peke yake hawezi kuifanya timu
ishinde lazima tujivunie kuwa na timu bora na kuimba nyimbo za ushindi
kila wakati.
|
No comments:
Post a Comment