Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda na Ujumbe wake wakioneshwa na
Ndg. Koichiro Maeda Mkurugenzi wa Makumbusho ya Hiroshima mchoro wa
madhara ya Bomu la Atomic lilirushwa katika Mji wa Hiroshima wakati wa
vita kuu ya pili mwaka 1954 jinsi mji huo ulivyokuwa siku hiyo baada ya
kulipuliwa.
Picha na Owen Mwandumbya wa Bunge
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda na Ujumbe wake wakitizama picha
iliyopigwa baada ya kulipuliwa Mji wa Hiroshima mwaka 1945 na Bomu la
Atomic. Picha hiyo ilipigwa tarehe 6 agosti 1945 mda mchache baada ya
kulipuliwa kwa mji huo.
Mhe. Tundu Lissu akiuliza swali kuhusu mda uliochukua kuujenga upya mji
huo
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akimsikiliza kwa makini mmoja wa
mashuhuda aliyenusurika katika Mlipuko wa Bomu la Atomic Mzee. Keijiro
Matsushima siku lilipoteketeza mji wa Hiroshima tarehe 6 Agosti 1945
ambapo zaidi ya watu 66,000 walifariki 92,000 hawakujulikana walipokuwa
mpaka sasa na 129,558 walijeruhiwa vibaya. Mzee Matsushima
alikuwa na umri wa miaka 16 siku hiyo na siku ya mlipuko alikuwa
darasani km 2 katika chuo cha Hiroshima Technical College ambapo katika
darasa alilokuwapo wanafunzi kadhaa walifariki pia kutokana na mionzi
mikali ya bomu hilo. Hivi sasa Mzee Matsushima ana miaka 83. Kushoto kwa
Mhe. Spika ni Mhe. Godfrey zambi na Mhe. Anne Kilango
Malecela
Shuhuda aliyenusurika katika Mlipuko wa Bomu la Atomic Mzee.
Keijiro Matsushima akiwaonesha katika ramani waheshimiwa Wabunge na Mhe.
Spika eneo alipokuwa siku bomu linalipuka na sehemu bomu lilopolipukia.
Mzee. Keijiro Matsushima akielezea kwa hisia jinsi alivyojikongoja
kuukimbia mji wa Hiroshima huku akipisha na mamia ya wakazi wa eneo
hilo wakio wanakimbia na huku ngozi zao zikinyofoka
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwa katika Picha ya Pamoja na Mzee.
Keijiro Matsushima shuhuda aliyenusurika katika Bomu la Atomic
lilisambaratisha mji wa Hiroshima
Jengo pekee lililosalia baada ya bomu la Atomic kutoa na
kusambaratisha mji wa Hiroshima. Hivi sasa jengo hilo limehifadhiwa kati
hali yake kwa kumbukumbu ya tukio
hilo |
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akimkabidhi Ndg. Koichiro Maeda
Mkurugenzi wa Makumbusho ya Hiroshima ujumbe kutoka kwa timu ya wabunge
aliongozana nayo ziara hiyo wenye kulaan matumizi ya silaha za Nuclear
Dunian.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akisaini kitabu cha Kumbukumbu na
kuandika ujumbe wa kulaani matumizi ya silaha za Nuclear baada ya
kumaliza kutembelea makumbusho yenye picha na matukio yaliyotokea siku
bomu la Atomic lilivyo sambaratisha mji wa Hiroshima
No comments:
Post a Comment