N.I.H.F -KIKOA

N.I.H.F -KIKOA
N.I.H.F -KIKOA

FOREPLAN CLINIC

FOREPLAN CLINIC
FOREPLAN CLINIC

Wednesday, May 9, 2012

MKUTANO WA MAJUMUISHO YA ZIARA YA RAIS DK. SHEIN WA ZANZIBAR

Wanakijiji wa kijiji cha Kipera wamtimua Afisa Mtendaji wa Kijiji chao

Mwenyekiti wa Kijiji cha Kipera, Anthony Karoli (wapili kushoto) akiwa katika maoja ya shunguli za kijiji jana.
 
 
Na Mwandishi wetu, Mvomero. 
 
KATIKA kuhakikisha viongozi wa Serikali wanawajibika na wanakua waadilifu katika utekelezaji wa shughuli zao kwa jamii ipasavyo, Halmashauri ya Kijiji cha Kipera Kata ya Mlali Wilayani Mvomero mkoani Morogoro, wamemtimua Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho, Fedinand Makunga kwa tuhuma mbalimbali.
Viongozi hao wa Kijiji walikutana mapema wiki hii chini ya Mwenyekiti Anthon Karolin a wakiwa katika mkutano wao wa kawaida wa Halmashauri hiyo ya kijiji iiliibuka Agenda ya kumkataa Mtendaji huyo na kumtaka akibidhi ofisi mara moja, kutokana na shutuma mbalimbali za kiutendaji dhidhi yake.
 Habari zilizoifikia blogu hii kutoka kwa wajumbe wa kikao hicho walidai kuwa wamefikia uamuzi huo kutokana na kuona utendaji mbovu wa Mtendaji huyo.

“Kiukweli huyu Mtedaji huyu hatufai na hatumtaki tena kijijini kwetu, maana amekuwa kero na kwa uongozi wa kijiji na matokeo yake wananchi wanaulala mikia uongozi wetu kuwa haufanyi kazi lakini kumbe anetukwamisha ni mtedaji wa Kijiji,” alisema mmoja wa wajumbe.
Mjumbe huyo ambaye hakutaka kutaja jina lake alidai kuwa miongoni mwa mambo ambayo anashutumiwa mtendaji huyo ni pamoja na uaminifu, kutokuleta maendeleo kijijini, na kuto tatua migogoro ya wananchi.
“Mtendaji amekuwa si mwaminifu maana amekuwa akipokea fedha kwa wananchi za michango lakini hazifikishi sehemu husika, na akiulizwa anakana kupokea fedha hizo ilhali mtoaji anathibitisha kumpatia,” alisema mjumbe Mwingine.

Pia Mtendaji Makunga, anashutumiwa kupokea rushwa kutoka kwa mwekezaji wa Kizungu wa sghamba la kinyenze ili asishughulikie tatizo la mgogoro wa ardhi kijijini hapo na badala yake kuwaambia wananchi kama wanataka kushughulikiwa kwa mgogoro huo wachange Shilingi hamsini elfu.
Pia inadaiwa kuwa miradi ya maendeleo iliyopo kijijini hapo ya Ujenzi wa soko na kiwanda cha kusindika nyanya na matunda ambavyo vilianza ujenzi wake na Afisa Mtendaji aliyefariki, hayati Ramadhan Maguo hajaviendeleza kwa zaidi ya miaka 3 sasa na akiulizwa anadai kuwa Kipera sio kijiji chake na hakuja hapo kuleta maendeleo.

Mbali na shutuma hizo pia Mtendaji huyo anadaiwa kuruhusu kuwekwa kwa geti la ukusanyaji ushuru kijijini hapo ambapo wananchi hata wakipita na mazao yao ya shambani yakwenda kula hutakiwa kulipa ushuru na ushuru huo hauna manufaa kwa kijiji kwakuwa unaenda halmashauri na Kijiji hakipati hata senti. 
Inadaiwa kuwa Mtendaji huyo alipotakiwa kuachia ngazi na kurudi kwa mwajiri wake na si kijijini hapo, alidai mbele ya baraza hilo la kijiji kuwa Kijiji hakina mamlaka ya kumfukuza hapo isipokuwa ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mvomero pekee.
Hata hivyo Viongozi hao ambao walichachamaa na kumtaka aondoke aende kwa huyo mwajiri wake na si Kipera maana mvomero ina vijiji vingi.
Kufuatia hatua hiyo wananchi wa Kipera wameupongeza uongozi wa kijiji chao na kuwataka wazidi kuwa wakali kwa viongozi ambao hawafanyi kazi zao na wamekuwa ni mzigo kwa kijiji.

MKUTANO WA MAJUMUISHO YA ZIARA YA RAIS DK. SHEIN WA ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) alipokuwa akizungumza na watendaji  wa Ofisi za Serikali Mkoa wa Kusini  Unguja, katika mkutano wa majumuisho uliofanyika katika ukumbi wa Chuo   Kikuu cha Zanzibar Tunguu leo ,baada ya kumaliziki kwa ziara  katika Mkoa huo . [Picha
na Ramadhan Othman,Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) alikifuatana na viongozi na kuingia
katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu cha Zanzibar Tunguu katika
mkutano wa  watendaji  wa Ofisi za Serikali Mkoa wa Kusini  Unguja,
katika mkutano wa majumuisho uliofanyika Chuoni hapo leo.baada ya
kumaliziki kwa ziara  ya Rais katika Mkoa huo . [Picha na Ramadhan
Othman,Ikulu.]
Baadhi ya  Viongozi na watendaji katika ofisi
mbali mbali za Mkoa wa Kusini Unguja,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa na
mazungumzo na watendaji hao katika mkutano wa majumuisho ya ziara
aliyoifanya katika Mkoa wa Kusini Unguja,mkutano huo ulifanyika leo
katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Zanzibar Tunguu,Wilaya ya  Kati
Unguja.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGA AWAMU YA KWANZA YA MAANDALIZI YA SENSA YA WATU NA MAKAZI, MKOANI TABORA LEO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyeshwa Ramani ya makazi itakayotumika na Makarani katika zoezi la kuhesabu Sensa ya watu na makazi, na kusikiliza maelezo kutoka kwa Kamishna wa Sensa, Hajat Amina Said Mrisho, wakati Makamu alipokuwa akifunga Awamu ya kwanza ya maandalizi ya sensa ya watu na makazi iliyofanyika leo Mei 9, 2012, Mkoani Tabora.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya Picha ya Ramani ya Tanzania, kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Ramani Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Vincent Mugaya, baada ya kufunga Awamu ya kwanza ya maandalizi ya sensa ya watu na makazi iliyofanyika leo Mei 9, 2012, Mkoani Tabora.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifunua kitambaa kuashiria kuhakiki Ramani ya iliyoandaliwa kwa zoezi la kuhesabu Sensa ya watu linalotarajia kuanza Tarehe  26 Mwezi Agosti, mwaka huu, wakati alipokuwa akifunga Awamu ya kwanza ya maandalizi ya Sensa ya watu na makazi iliyofanyika leo Mei 9, 2012, mkoani Tabora.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia wananchi wa Mkoani Tabora wakati akifunga Awamu ya kwanza ya maandalizi ya sensa ya watu na makazi iliyofanyika leo Mei 9, 2012 katika Uwanja wa Chipukizi mkoani Tabora.
Makamu akiwasili kwenye uwanja wa chipukizi mkoani tabora kufunga awamu ya kwanza ya maandalizi ya  sensa ya watu na makazi iliyofanyika leo Mei 9, 2012 katika Uwanja wa Chipukizi mkoani Tabora.

MAWAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII WAANZA KAZI RASMI

Naibu Waziri wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Seif  Rashid  akisalimiana na kaimu Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Donan Mmbando mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Wizara huyo, kushoto kwake ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara Bi. Regina Kikuli
Naibu Waziri Mh.Dkt Rashid akiwapungia mikono kuwasalimia watumishi wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Mh. Dkt. Hussein Mwinyi akisalimiana na baadhi ya watumishi wa wizara yake mpya
Mh. Dkt. Mwinyi akipokea vitendea kazi mara baada ya kuwasili rasmi kwenye ofisi yake mpya ya Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii.Dkt Mwinyi amewataka wakurugenzi wa Idara,Taasisi, Wakala pamoja na wakuu wa Idara kuwa na ushirikiano ili kuweza kutatua changamoto zilizopo kwenye wizara hiyo, aidha wawe makini na kasoro ndogondogo ili kuweza kuwa na majibu mazuri yatakayoweza kukidhi mahitaji ya wananchi
Naibu Waziri Mh.Dkt. Rashid akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuripoti kwenye wizara hiyo.

Makampuni yatakiwa kuacha tabia ya kutumia nembo ya msalaba mwekundu



Na Gladness Mushi -Arusha

MAKAMPUNI na taasisisi mbali mbali mkoani Arusha yametakiwa kuacha kutumia nembo ya shirika la msalaba mwekundu kwa kuwa kutumia nembo hiyo ni kinyume na taratibu za sheria.
Hayo yalisemwa juzi na mratibu wa wa chama cha msalaba mwekundu mkoa wa arusha Bbi Sophia Senkondo wakati akiongea katika maadhimisho ya kumbukumbu ya muhasisis wa shirika hilo yaliyofanyika katika uwanja wa sheik Amri mjini hapa.


Bi Senkondo alisema kuwa yapo baadhi ya mashirika na taasisis mbali mabli zimekuwa zikitumia nembo yao bila idhini yao jambo ambalo amesema kuwa ni kinyume na sheiria hivyo hawana budi kuacha kutumia mara moja.

Aidha mratibu huyo alitaja baadhi ya taasisis hizo na mashirika kuwa ni pamoja na mahospitali,maduka ya  dawa baridi  , na mengineyo mengi ambapo alisema kuwa matumizi ya nembo hiyo katika mashiriika hayo ni kinyume na sheria kutokana na kutokuwa na kibali kutoka katika shirika hilo.
Hata hivyo bi Sophia aliitaka serikali kubadilisha sheria ya mwaka 1962  namba 71 na kuweka sheria ingine kali itakayoweza kuwathibiti wale wote wanaotumia nembo hiyo pasipo na kibali maalum cha kutumia.
Aidha gazeti hili lilifanikiwa kuongea na bi Diana Mmbaga ambaye ni mmoja wa wauguzi katika kituo cha afya cha Trust kilichopo maeneo ya kaloleni ili kubaini ni kwa namna gani wanatumia nembo hiyo ambapo alisema kuwa hawana elimu sahihi juu ya nembo hiyo hivyo kulitaka shirika hilo kutoa elimu ya kutosha kwa taasisi zinazotumia nembo hiyo kimakosa na kwa wananchi kwa hujumla.
Mmbaga alisema kuwa ni wazi kuwa watumiaji wengi wanaotumia nnembo hiyo hawatumii kimakosa na hawajui kama kuitumia ni kinyume hivyo endapo elimu itatolewa juu ya nembo hiyo ni wazi kuwa haitatumika tena kimakosa.

WAZIRI MKUU PINDA AKUTANA NA UJUMBE WA TUME YA KURATIBU MAONI YA KATIBA NA KAMPUNI YA STATOIL

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiagana na Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe baada ya kutembelea Ofisi za Tume Kamati ya Mabadiliko ya Katiba   na kuzungumza na wajumbe wake, jijini Dar es salaam May 9, 2012.Kulia niMwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Joseph Sinde Warioba. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mwenyekiti wa Tume  ya Kamati ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Sinde Warioba  na wajumbe wa Tume hiyo baada ya kutembelea Ofisi za Tume jijini Dar es salaam May 9, 2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na  Rais  wa Kampuni ya Mafuta ya STATOIL sna ujumbe wake, ofisini kwake jijini Dar es salaam May 9, 2012. (Picha na Ofisi ya WaziriMkuu)

No comments:

Post a Comment

Blog Archive