N.I.H.F -KIKOA

N.I.H.F -KIKOA
N.I.H.F -KIKOA

FOREPLAN CLINIC

FOREPLAN CLINIC
FOREPLAN CLINIC

Thursday, May 17, 2012

WASHIRIKI TANZANIA KATIKA INDABA WAFURAHIA MAFANIKO


 Baadhi ya washiriki wa maonesho ya INDABA kutoka Tanzania wakiwa katika majadiliano ya kibiashara na wafanyabiasha wenzao katika sekta ya utalii kutoka nchi mbalimbali pamoja na watu mbalimbaliwanaoshiriki na kutembelea Banda la Tanzania katika maonesho ya INDABA Durban Afrika Kusini.

Na: Geofrey Tengeneza, Durban
 Wafanyabiashara katika sekta ya utalii kutoka Tanzania waliokuwa wakishiriki katika maonesho ya kimataifa ya INDABA yaliyokuwa yakifanyika Durban nchini Afrika Kusini wameeleza kuridhishwa kwao na tija iliyopatikana kwa kushiriki kwao katika maonesho hayo ikiwa ni pamoja na kufanikiwa kuanzisha mahusiano na wafanyabiashara wenzao katika sekta hiyo kutoka nchi mbalimbali duniani.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa nyakati tofauti ndani ya  banda la Tanzania katika maonesho hayo hivi karibuni mjini Durban Afrika Kusini, washiriki hao wamesema kupitia maonesho hayo wameweza kukutana na wamiliki au wawakilishi wa makampuni yanayojihusisha na biashara zinazohusiana na utalii na wadau wengine wa utalii kutoka mataifa mbalimbali duniani na kufanikiwa kuanziosha mchakato wa kufikia makubaliano ya ushirikiano baina yao jambo ambalo wamesema litasaidiza kukuza biashara zao na kuitangaza zaidi Tanzania katika katika tasnia ya utalii duniani. Aidha wamesema kupitia maonesho hayo wameweza pia kupata watu kadhaa ambao wameonyesha dhamira ya kuja Tanzania kutembelea vivutio vya kitalii na kutumia huduma zao.
Kwa upande wake Mkurugenzi mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania Dk. Aloyce Nzuki amepongeza makampuni yote katika sekta binafsi na taasisi za serikali zilizojitokeza kushiriki katika maonesho hayo chini ya uratibu wa Bodi ya Utalii Tanzania kwa namna walivyotekeleza wajibu wao kikamilifu si tu kutangaza biashara zao lakini pia katika kuitangaza vema Tanzania sambamba na vivutio vyake vya utalii kiasi cha kulifanya banda la Tanzania kuwa miongoni mwa mabanda yaliyovutia watu mbalimbali katika maonesho hayo “ Bodi ya Utalii kwa ujumla tumefurahishwa sana na namna makampuni katika sekta binafsi na taasisi za umma tulivyoshirikiana na kushikamana kwa pamoja katika kuitangaza Tanzania” anasema Dk Nzuki
Maonesho hayo makubwa kuliko yote barani Afrika na ambayo hufanyika kila mwaka jijini Durban Afrika Kusini mwaka huu yalianza tarehe 12/5/2012 na kumalizika 15/5/2012 huku Tanzania iliwakilishwa na makampuni 49 kutoka sekta binafsi na taasisi sita za umma. Katika maonesho kama haya mwaka jana Banda laTanzania lilitunukiwa tuzo ya kuwa Banda Bora kuliko yote katika maonesho hayo miongoni mwa nchi za SADC.

ZUKU ANNOUNCES ONE MILLION DOLLAR SPONSORSHIP OF ZIFF




ZUKU today announced its headline event sponsorship of the Zanzibar International Film Festival for a period of 10 years from 2012 to 2022 inclusive, with a focus on supporting ZIFF’s film and festival promotion and marketing program.
The sponsorship, which is for a period of ten year’s will be for $100,000 per annum and will include an incremental raise.
Wananchi Group CEO, Richard Bell, said the agreement represented a significant step forward for the partnership, which would see ZUKU become headline sponsor of ZIFF. “Of course, as the festival grows and develops we may both see different needs and opportunities - but this should give us a solid footing to start on”, he said.
We do not, however, mean to lock out other sponsors/contributors and collaborators. On the contrary, we would hope that our long term involvement would help attract greater consistency from other partners.”
Lauding the momentous occasion Chairman of Wananchi Group, Ali Mufuruki added, "As a broadcaster, ZUKUis deeply invested in the growth and success of East Africa's creative and content industries. It is therefore with pride that we enter into this association with ZIFF, which has for the last 15 years been instrumental in celebrating and enabling film making from the region and around the world." 
Speaking of partnership from Geneva, the ZIFF Chairman, Mr.Mahmoud Thabit Kombo said he had been overwhelmed by the high level of confidence in the company’s sponsorship of ZIFF. “ZIFF is a huge part of African culture and as a proud Zanzibari organisation we are pleased to extend this great relationship,” he said.
ZUKU’s initial ten-year agreement concludes at the end of the 2022 season and The ZIFF chair said the partnership would by then have evolved into a strong business and community relationship.
“While we like seeing the ZUKU logo side by side with ZIFF, our partnership goes well beyond branding,” he said. “As ZUKU spreads its wings to capture the pay TV market in East and Central Africa, ZIFF will work closely together with ZUKU to develop the film and media entertainment industry”.
The partnership is a beacon of innovative marketing for investors and entrepreneurs who have a vision for economic growth and employment creation in all sectors, especially tourism and entertainment. Working to promote the local creative industries, ZIFF and ZUKU will help create employment opportunities for filmmakers, producers and actors throughout the region. 
“ZUKU is the fastest growing Pay TV provider in East Africa, aiming to offer high-quality, affordable home entertainment services. It is currently available in Tanzania, Kenya and Uganda with plans to roll out to neighboring countries."
ZIFF will take place between 7th and 15th July 2012.

TANZANIA MWENYEKITI WA KAMATI YA DUNIA YA SAYANSI NA TAALUMA YA MABADILIKO YA TABIA NCHI


Bw. Richard Muyungi katikati Mkurugenzi msaidizi wa Idara ya mazingira ofisi ya makamu wa rais baada tuu ya kupewa uwenyekiti wa kamati ya dunia ya sayansi mabadiliko ya tabia nchi, huko Durban africa ya kusini na kuanza kazi rasmi katika mutano unaendelea hapa ujerumani. (Evelyn Mkokoi)
Mkurugenzi msaidizi wa Idara ya Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais bw. Richad Muyungi akiwa katika Ofisi yake mjini Bonn Ujerumani akiiwakilisha Tanzania kama mwenyekiti wa kamati ya dunia ya Sayansi na taaluma ya mabadiliko ya tabia nchi, kazi hiyo ameianza rasmi katika mkutano wa mabadiliko ya tabia nchi unaoendela hapa Bonn Ujerumani,(Evelyn Mkokoi)
Evelyn Mkokoi
Afisa Habari
Ofisi ya Makamu wa Rais
Bonn, Ujerumani
 Tanzania kwa mara ya kwanza imepata nafasi kwa  miaka miwili ijayo ya kuongoza   Kamati ya umoja wa mataifa ya sayansi na taaluma ya mabadiliko ya tabia nchi, chini ya mkataba wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabia Nchi. Kamati imeanza kazi rasmi jana wiki hii,  wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 36 wa mabadiliko ya tabia nchi. Hayo yameelezwa leo katika mahujiano maalum na ofisa Mkuu wa programu ya Uendeshaji ya Sekretarieti ya Mkataba huu Bi Hanna Hoffmann, hapa Bonn, Ujerumani.
Bi Hanna Ameeleza kuwa Bw. Richard Muyungi ambae ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya mazingira kutoka katika ofisi ya Makamu wa Rais amepewa dhamana hiyo na nchi zote duniani wanachama wa mkataba huu kutokana na uzoefu wake mkubwa katika  diplomasia ya  mabadiliko ya tabianchi na upeo wa kutosha juu ya taaluma nzima ya sayansi ya mabadiliko ya tabianchi. “Bw. Muyungi ni mwana diplomasia aliyebobea katika masuala ya mabadiliko ya tabianchi, ana elimu ya kutosha katika eneo hili na ni mzoefu sana na amekuwa akihudhuria na kuongoza mkutano mingi ya mabadiliko ya tabianchi hasa zaidi akiongoza kundi la nchi zinazoendelea, hivyo naamini kabisa, uteuzi wake ni muafaka na ataongoza vizuri kamati hii na masuala yote muhimu kama ulivyoona mwenyewe alivyoongoza leo mkutano kuhusu kilimo na mabadiliko ya tabianchi .” Alisisitiza.
Bi Hanna aliongeza kuwa Kundi la nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania ina nafasi kubwa zaidi ya kujifunza na kutumia njia za kuhimili na kukabilina na mabadiliko ya tabia nchi zaidi kutokana na nafasi yake ya uwenyekiti wa Kamati hii.
 Kwa Upande wake Bw. Richard Muyungi ameeleza kuwa uteuzi huu uliofanyika rasmi Desemba mwaka jana na nchi zote wanachama huko Durban  Afrika ya kusini, na kuanza rasmi leo, ni heshima  kwa nchi  na nafasi ya pekee kwa Tanzania kuweza  kujifunza mengi  na kupata fursa  mbali mbali za kuweza  kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi zinazoikabili  Tanzania ikiwemo uhaba wa mvua, mafuriko, kuongezeka kwa kina cha bahari na,  mvua zisizotarajiwa, na baadhi ya maeneo ya nchi kuelekea kuwa janga kutokana na mabadiliko haya.
Mkutano huu unaoendelea hapa  mjini Bonn Ujerumani, ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano wa Dunia wa mabadiliko ya tabia nchi, ambao utawakutanisha wakuu wa nchi duniani utakaofanyika mjini Doha,Qatar, Novemba mwaka huu. Aidha utatoa mchango katika mkutano wa wakuu wa nchi kuhusu Maendeleo endelevu (Rio+20) utakaofanyika huko Rio, nchini Brazil baadaye mwezi Juni.
Pamoja na masuala ya Kilimo na mabadiliko ya tabianchi, Kamati hii pia inatafuta muafaka kuhusu suala la matumizi ya sekta ya misitu katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa kuzingatia maslahi ya nchi zenye misitu inayonyonya gesi hizi, na taratibu za kusimamia na kutekeleza miradi ya kupunguza hewa ukaa  katika nchi zinazoendelea bila kuathiri maendeleo ya nchi hizi. Aidha katika mkutano huu, Masuala ya upatikanaji wa fedha ili kukabiliana na mabadilkio ya tabianchi kwa nchi maskini duniani na suala la nchi zilizoendelea kuongeza juhudi za kupunguza gesijoto zinazosababisha mabadiliko ya tabianchi yamepewa kipaumbele.

Musician Recaptures Tanzanians Lost Glory


Tanzania has regained its lost glory in world of music fame that has dwindled since the eighties.
When the name of Tanzania is currently mentioned in international music circles the name of Ebrahim Makunja popularly known as Ras Makunja of FFU and his “The Ngoma Africa Band” aka FFU based in Germany cannot be slighted. FFU has earnestly strived to place Tanzania in the international music charts.
 
It is the only Tanzanian band that is based overseas. Its contribution in the music industry both in Tanzania, East Africa and abroad is superb. The band has often been able to bring its records to radio stations back at home.
Many of their hits touch the souls of their fans. Two of their hits, which are very popular in local radio stations and contained in “50 Uhuru Anniversary” CD are “Shangwe”, and “Miaka 50 ya Uhuru”. The rumba style songs are composed by band leader Ras Makunja.
He pairs in singing with the comical solo guitarist Chris-B. Apart from the well composed lyrics and the highly perfected musical beat the songs carry very strong and emotional messages to the community. Their messages are acclaimed not only in Tanzania but world all over.
Ras Makunja of FU, is not only a seasoned tactful and artistic composed. He too has visionary messages to the society. To call him Kamanda (Commander) Ras Makunja is not demeaning him.
He ensured that two of his CDs including “Jakaya Kikwete 2010″ which claimed global fame reached more than 310 radio stations in the world. This CD earned him the mark of being a hard headed musician from some quarters.
His band now dubbed FFU (Fanya Fujo Uone) literally means creates chaos and see, immediately came up with a CD “Anti Corruption Squad” which has the song “Rushwa ni Adui wa Haki”. The fans see this song as the Al-Albadir of the corrupt.
The song was a smash hit within Tanzanians. It placed Ras Makunja and his band ‘Ngoma Afrika’ not only as ordinary musicians in the musical arena. They had something else to offer the society apart from the usual entertainment. Visionary eye opening and soul searching messages.
Yet despite all this no one seems to realize the onerous task that this musicians does. They have never been ordained with a single medal here at home. As a popular Swahili goes “Asiyekuwepo na lake halipo” (He who is not there (present) so is his/her share). Ras Makunja and Ngoma Afrika may not be with us, but his works and messages are!
The official web of the band is www.ngoma-africa.com One can become a fan member of the band by signing up. The good work the band is doing in promoting Tanzania in the field of music deserves local support both in cash and form.

ICTR KUTOA HUKUMU YA KAPTEINI NIZEYIMANA JUNI 19

ASHURA MOHAMED-ARUSHA

Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) itatoa hukumu ya kesi inayomkabili afisa wa zamani wa jeshi la Rwanda, Kapteni Idelphonse Nizeyimana Juni 19, 2012, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mahakama hiyo Ijumaa.
 
Nizeyimana anakabiliwa na mashitaka ya mauaji ya kimbari, kuteketeza kizazi, mauaji na ubakaji.
Mwendesha mashitaka pamoja na mambo mengine anadai kwamba mshitakiwa alikuwa mtu wa pili kimadaraka  aliyekuwa anashughulikia Usalama na Operesheni za Kijeshi katika Chuo cha Maafisa wa Jeshi Wasiokuwa na Kamisheni (ESO), mkoani Butare, Kusini ya Rwanda.
Nizeyimana anadaiwa kuamuru, kusimamia na kupanga mauaji dhidi ya Watutsi katika maeneo mbalimbali mkoani humo ikiwa ni pamoja na mauaji dhidi ya Malkia wa Kitutsi, Rosalie Gicanda Aprili 21, 1994.
Katika kuwasilisha hoja za mwisho Desemba 7, 2011, mwendesha mashitaka aliiomba mahakama iliyokuwa inaongozwa na Jaji Lee Muthoga, kumpatia adhabu ya juu kabisa inayoweza kutolewa na mahakama hiyo ya kifungo cha maisha jela iwapo atatiwa hatiani.
‘’Adhabu pekee muafaka kwa mujibu wa mwendesha mashitaka ni kumpatia kifungo cha maisha jela ,’’ alipendekeza Mwendesha Mashitaka, Drew White.
White pia hakulifumbia macho suala la madai ya kuhusika kwa mshitakiwa katika mauaji dhidi Malkia wa Kitutsi, Rosalie Gicanda kwa kueleza kwamba, mashahidi wawili wa kuaminika wa upande wa mwendesha mashitaka walitoa ushahidi wao akiwemo mjukuu wake na mpishi.
Hata hivyo, John Philpot, Wakili Kiongozi wa Nizeyimana alipangua hoja za mwendesha mashitaka kwa kusema kuwa ameshindwa kuthibitisha mashitaka dhidi ya mteja wake pasipo mashaka. Alisema kwamba mteja wake alichukua hatua sahihi zilizopaswa kuchukuchukiwa na askari nyakati za vita.
‘’Mteja wangu hakuwa kiongozi wa ESO, hakuwa na mamlaka kamili na hakuwa na mamlaka ya kisheria juu ya askari waliodaiwa kuwa chini ya himaya yake,’’ alisema wakili huyo.
Pia wakili huyo aliwasilisha ushahidi wa kuwa mteja wake wakati fulani hakuwepo katika maeneo yalikofanyika uhalifu kwenye miezi ya Aprili na Mei, 1994 bali muda huo alikuwa katika kiwanda cha Chai cha Mata, mkoani Gikongoro akiendesha mafunzo ya kijeshi kwa askari wapya.
‘’Kesi hii sasa iko mikononi mwenu. Tunawaomba kusimama katika ukweli na haki kumwachia huru Nizeyimana,’’ Nizeyimana aliwaomba majaji alipokuwa anakamilisha kuwasilisha hoja zake za mwisho.
Nizeyimana alitiwa mbaroni nchini Uganda, Oktoba 5, 2009 na kuhamishiwa katika gereza la Mahakama ya Umoja wa Mataifa Arusha, Tanzania, siku iliyofuata. Alikana mashitaka dhidi yake alipofikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Oktoba 14, 2009.
Kesi yake ilianza kusikilizwa Januari 17, 2011 ambapo mwendesha mashitaka aliita mashahidi 38 na upande wa utetezi pia uliita idadi sawa na hiyo na kufunga kesi yake Februari 25, 2011.

No comments:

Post a Comment

Blog Archive