KUTOKA KATIKA MTANDAO WETU WA MAJIRA GAZETI LA KILA SIKU
Posted: 04 May 2012 02:15 AM PDT
|
Posted: 04 May 2012 01:45 AM PDT
*Wamo Profesa Muhongo, Bi. Janet Mbene *Watabiriwa kuwemo kwenyea baraza jipya *Nchimbi awaomba Watanzania wamuombee *Tibaijuka, Magufuli nyota zao zang'aa
WAKATI
Rais Kikwete anatarajia kufanya mabadiliko katika baraza kake la
mawaziri wakati wowote sasa, jana amemteua Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi,
Bw. James Mbatia, kuwa mbunge.
Mbali
na Bw. Mbatia, Rais Kikwete amemteua Profesa safi Profesa Sospeter
Muhongo, Bi. Janet Mbene, kuwa wabunge. Taarifa iliyotolewa kwenye
vyombo vya habari jana Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, ilieleza kuwa Rais Kikwete amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa mamlaka ya uteuzi aliyopewa.
"Rais
Kikwete amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa mamlaka ya uteuzi aliyo nayo
chini ya Ibara ya 66(i) (e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
Uteuzi huo
umetafsiriwa na wachambuzi wa masuala ya kisiasa kuwa watu hao
wanaandaliwa kuwa mawaziri, hasa ikizingatiwa kuwa Rais anatarajiwa
kufanya mabadiliko ya baraza lake wakati wowote kuanzia sasa.
Profesa
Muhongo ambaye ni mtaalam wa masuala ya madini Geology anatabiriwa
kukabidhiwa kuongoza Wizara Nishati na Madini, huku nafasi za wengine
walioteuliwa zikiwa bado kitendawili.
Akizungumza na gazeti hili
Dar es Salaam jana Mhadhiri wa Kitivo cha Sayansi za Siasa katika Chuo
Kikuu cha SAUT, Profesa Mwesiga Baregu, kuhusu uteuzi huo, alisema;
"Anawaandaa kwa ajili ya kuwaweke katika baraza lake la mawaziri."
Profesa
Baregu alisema alisema baraza la mawaziri la sasa limepwa ndiyo maana
ameamua kuchukua watu kutoka nje ya CCM. Alimshauri Rais Kikwete, kuteua
baraza la mawaziri lenye sura mpya na watu wachache na wenye uwezo wa
kufanyakazi.
Alitaja sifa nyingine ambazo anataka mawaziri wapya
kuwa nazo kuwa ni uaminifu, wawajibikaji, uadilifu na wenye kuleta tija
kwa wananchi wanaowatumikia.
"Akichagua wale wale wa zamani
hakutakuwa na mabadiliko yoyote," alisema Profesa Baregu. Alishauri
mabadiliko hayo ya baraza yafanyike haraka kwani kuwaacha wanaotuhumiwa
kwa kushindwa kuwajibika kuendelea kuwepo ofisini kunaweza kuwapa
mwanya wa kupoteza vielelezo pindi watakapofikishwa kwenye vyombo vya
sheria.
"Mimi namshauri rais kufanya mabadiliko haraka
iwezekanavyo, kwani kuendelea kuwepo ofisini kwa mawaziri hao ni tatizo
na mambo yanaweza kuharibika kwa kuwa wana uwezo wa kuchukua vielelezo
na kupoteza ushahidi," alisema.
Hata hivyo alisema kufanya
mabadiliko pekee hakutasaidia bali kinachotakiwa ni kuwatendea haki
mawaziri hao kwa kuwafikisha mahakamani ili watakaobainika.
Alisema
mbali na kubadilisha baraza la mawaziri, pia anatakiwa kuwachukulia
hatua wote waliohusika wakiwemo makatibu wakuu wa wizara kama
wanahusika.
Alisema upotevu wa fedha ni matokeo ya kukosekana kwa
uwajibikaji miongoni mwa mawaziri hao. Alipoulizwa ni mawaziri wapi
wanafaa kubaki kwenye safu mpya itakayoundwa, alisema atatoa maoni yake
baada ya uteuzi.
Naye, Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za
Binadamu (LHRC) Dkt. Helen Kijo- Bisimba, alisema kubadilisha mawaziri
si suluhuhisho kukabiliana na tatizo la viongozi kutowajibika.
Alisema kuwa suluhu ni kuwawajibisha wale wote waliohusika na kwa kuwfaikisha mahakamani ili haki itendeke.
Kuhusu
makatibu wakuu wambao ndio watendaji, Dkt. Kijo-Bisimba alisema kuwa
mawaziri hao walitakiwa kuwawajibisha makatibu wakuu pale wanapoona
kwamba hawarishishwi na utendani wao wa kazi kwa kuwa wao ndio wapo
nafasi za juu kiutendaji.
Mwenyekiti wa Chama cha PPT-Maendeleo,
Bw. Peter Mziray, alisema wabunge wamemweka Rais Kikwete kwenye kona
mbaya, hivyo ni lazima afanye mabadiliko kwa kuteua mawaziri ambao
wananchi wanawaamini.
Pia alishauri baraza atakalounda Rais
Kikwete, liwe dogo, kwani la sasa ni kubwa kiasi kwamba inawezaka wakati
mwingine akashindwa kuwafahamu.
"Ndiyo maana waziri anaweza kuwa
na mali nyingi, lakini akashindwa kufahamu kwa sababu hana muda wa
kuwafuatilia," alisema Bw.Mziray.
Aliwataja mawaziri wanaofaa
kuwemo kwenye baraza hilo kuwa ni Profesa Anna Tibaijuka, Dkt. John
Magufuli, Dkt. David Matayo, Bw. Bernard Membe na Bw. Shamsa Vuai
Nahodha.
Wakati huo huo Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Dkt. Emanuel Nchimbi, amewaomba Watanzania kumuombea ili aweze
kuteuliwa tena kurudi kwenye baraza la mawaziri.
Alisema bado ana moyo wa kuwatetea Watanzania katika mambo mbalimbali ili kuijenga nchi hii.
"Bado
ninahitaji kuwasaidia Watanzania wenzangu na ninawapenda, ndiyo maana
leo hii tena muda kama huu ambapo mawaziri wengi wapo katika sala za
kumuomba Mungu wao ili waweze kupita tena, lakini mimi nimeamua kuja
kwenu kwa ajili ya upendo wangu na ni moja ya kazi yangu,"alisema, Dkt.
Nchimbi.
Aliongeza kusema kuwa angeweza kumtuma hata mwakilishi
wake ili afike katika hafla ya uzinduzi wa mwongozi wa wamiliki na
mameneja wa vyombo vya habari, lakini kwa kuwa anafahamu maana yake,
ndiyo maana ameamua kufika mwenyewe.
Naye, Mwenyekiti wa Chama
cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT) Bw. Regnald Mengi
alimpongeza Dkt. Nchimbi kwa ujasiri wake wa kufika katika uzinduzi huo
wakati mawaziri wengine hadi hivi sasa wapo matumbo joto wakiangaika
huku na kule ili majina yao yaweze kupitishwa.
"Nakupongeza Dkt.
Nchimbi kwa ushujaa ulioonesha ni mkubwa na mawaziri wengi sasa hivi
matumbo joto kwa ajili ya kusikiliza kitakachotokea, tunakuona ni
jasiri, "alisema Bw. Mengi.
|
Posted: 04 May 2012 01:37 AM PDT
Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Zanzibra Bw. Ali Juma Shamuhuna
akizungumza na wananchi kabla ya kumkaribisha Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, ili awasalimie
wananchi wa Matemwe Kigomani, wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi
madarasa mpya katika shehia hiyo. Rais alikuwa katika ziara ya kuangalia
maendeleo ya miradi mbali mbali ya kijamii Wilaya ya Kaskazini A.
(Picha Ikulu Zanzibar)
|
Posted: 04 May 2012 01:27 AM PDT
|
Posted: 04 May 2012 01:21 AM PDT
Na Theonestina Juma, Kagera
WAANDISHI
wa habari mkoani Kagera wametakiwa kuwa makini katika kuelimisha jamii
juu ya rushwa kutokana vitendo hivyo huathiri zaidi wananchi maskini kwa
kushindwa kupata haki zao.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkuu wa
Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera Bw. Samuel Kamote wakati akifungua
mafunzo ya siku tatu ya waandishi wa habari wanachama wa Kagera Press
Club (KPC) wapatao 34 yaliyodhaminiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana
na Rushwa nchini (TAKUKURU) yanayofanyika mjini Bukoba.
Alisema,
kutokana na vitendo vya rushwa kuathiri zaidi wananchi maskini kwa
kuwakosesha kupata haki zao, hivyo waandishi wa habari wanalo jukumu na
nafasi kubwa ya kuelimisha wananchi kuhusu wajibu na namna ya kuepuka
rushwa.
Alisema, jamii inategemea waandishi wa habari kupitia
vyombo vyao vya habari kupata ufafanuzi mbalimbali wa rushwa na hivyo
wanatakiwa kuwa makini wanapoandika masuala ya rushwa ambayo
yasipoandikwa na kutangawa kwa usahihi, yanawachang’anya wananchi.
Aidha,
Bw. Kamote aliwataka waandishi hao kuwa waadilifu na waaminifu pindi
wanapoandika habari zao kwa kuzingatia maadili ya taaluma yao.
Pia
aliwasihi wanahabari hao kutoingilia kesi ambazo zinachunguzwa na
TAKUKURU kwa vile kufanya hivyo huathiri mwenendo mzima wa uchunguzi
wao.
Alisema, waandishi hao wanatakiwa kujielimisha zaidi na kufahamu vizuri sheria za kupambana na kuzuia rushwa ya mwaka 2007.
Aidha,
kwa upande wa Kamanda wa TAKUKURU mkoani Kagera Bi. Domina Mukama
alisema lengo la mafunzo hayo ni kukuza uelewa kwa waandishi wa habari
juu ya rushwa ili kuweza kufahamisha umma juu ya suala hilo.
Alisema,
mafunzo hayo ni mwendelezo wa mipango ya TAKUKURU katika kushirikiana
na vyombo vya habari ili kuwawezesha waandishi wa habari kuandika kwa
usahihi taarifa zinazohusu rushwa.
|
Posted: 04 May 2012 12:50 AM PDT
Na Theonestina Juma, Kagera
WAANDISHI
wa habari mkoani Kagera wametakiwa kuwa makini katika kuelimisha jamii
juu ya rushwa kutokana vitendo hivyo huathiri zaidi wananchi maskini kwa
kushindwa kupata haki zao.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkuu wa
Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera Bw. Samuel Kamote wakati akifungua
mafunzo ya siku tatu ya waandishi wa habari wanachama wa Kagera Press
Club (KPC) wapatao 34 yaliyodhaminiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana
na Rushwa nchini (TAKUKURU) yanayofanyika mjini Bukoba.
Alisema,
kutokana na vitendo vya rushwa kuathiri zaidi wananchi maskini kwa
kuwakosesha kupata haki zao, hivyo waandishi wa habari wanalo jukumu na
nafasi kubwa ya kuelimisha wananchi kuhusu wajibu na namna ya kuepuka
rushwa.
Alisema, jamii inategemea waandishi wa habari kupitia
vyombo vyao vya habari kupata ufafanuzi mbalimbali wa rushwa na hivyo
wanatakiwa kuwa makini wanapoandika masuala ya rushwa ambayo
yasipoandikwa na kutangawa kwa usahihi, yanawachang’anya wananchi.
Aidha,
Bw. Kamote aliwataka waandishi hao kuwa waadilifu na waaminifu pindi
wanapoandika habari zao kwa kuzingatia maadili ya taaluma yao.
Pia
aliwasihi wanahabari hao kutoingilia kesi ambazo zinachunguzwa na
TAKUKURU kwa vile kufanya hivyo huathiri mwenendo mzima wa uchunguzi
wao.
Alisema, waandishi hao wanatakiwa kujielimisha zaidi na kufahamu vizuri sheria za kupambana na kuzuia rushwa ya mwaka 2007.
Aidha,
kwa upande wa Kamanda wa TAKUKURU mkoani Kagera Bi. Domina Mukama
alisema lengo la mafunzo hayo ni kukuza uelewa kwa waandishi wa habari
juu ya rushwa ili kuweza kufahamisha umma juu ya suala hilo.
Alisema,
mafunzo hayo ni mwendelezo wa mipango ya TAKUKURU katika kushirikiana
na vyombo vya habari ili kuwawezesha waandishi wa habari kuandika kwa
usahihi taarifa zinazohusu rushwa.
|
Posted: 04 May 2012 12:39 AM PDT
|
Posted: 04 May 2012 12:28 AM PDT
|
Posted: 04 May 2012 12:24 AM PDT
Na Yusuph Mussa, Tanga
BAADHI
ya madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga wamesema
fedha za miradi zinazopelekwa kwa wananchi kwa ajili ya miradi ya
maendeleo ni kidogo ukilinganisha na kiwango kilichoidhishwa kwenye
bajeti, hivyo madiwani hao kuonekana ni waongo mbele ya jamii.
Hayo
yalisemwa jana kwenye mafunzo ya siku tatu kwa madiwani hao
yanayoratibiwa na halmashauri kwa uwezeshaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), ambapo Diwani wa Kata
ya Mgwashi Bw. Bakari Kavumo alisema kutopeleka fedha hizo ni kuwahadaa wananchi.
"Kila
tunapopitisha bajeti na Serikali kukubali kiwango cha fedha za kuleta
kwenye halmashauri, Hazina haileti fedha hizo kwa wakati uliopangwa,
lakini kibaya zaidi fedha zinaletwa kidogo tofauti na tulizoidhinishiwa
kwenye bajeti," alisema Bw. Kavumo.
Diwani wa Kata ya Mtae Bw.
Said Shehiza alisema madiwani bado hawajapewa meno ya kutosha kuwa
walinzi wa fedha za halmashauri, kwani baadhi ya mikataba wao
hawahusishwi.
"Madiwani tunaambiwa halmashauri ni yetu, lakini tumewekewa mipaka tunaambiwa tusiingie jikoni, hivyo tunashindwa kujua kinachoendelea kwenye mambo mengi," alisema Bw. Shehiza.
Diwani
wa Kata ya Mamba, ambaye pia ni Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Lushoto Bi.
Zubeda Titu alisema falsafa ya CCM kuwa Diwani ni figa la tatu haina
maana kwao, kwani figa hilo limeonekana kama ngazi tu ya kumuwezesha
Mbunge na Rais kupata madaraka.
"Figa la tatu ambalo ni sisi
madiwani ni la kukanyagia ili mafiga mengine yapande. Diwani analipwa
sh. 120,000 kwa mwezi, Mbunge pamoja na kulipwa mamilioni ya fedha bado
akipewa uwaziri anafanya mambo ya kifisadi... Serikali ni lazima
iangalie maslahi yetu na sisi madiwani," alisema Bi. Titu.
Mwezeshaji wa mafunzo hayo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tanga Bw. Yohana Miwa akitoa
mada alisema Diwani ni mwakilishi wa wananchi, hivyo anatakiwa akutane
mara kwa mara na waliomchagua ili kuchukua maoni yao na kuyafanyia kazi
kwenye ngazi mbalimbali.
Akizungumza na mwandishi, Makamu
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto ambaye pia ni Diwani wa
Kata ya Dule- Bumbuli Bw. Sebarua Shemboza alisema Rais Kikwete amepiga
'Ikulu' baada ya kuwaondoa wakaguzi wa ndani kwenye halmashauri.
"Kama
kuna jambo ambalo Rais Kikwete ameonesha nia ya dhati ya kufanya
maboresho katika kudhibiti fedha za umma kutumika visivyo kwenye
halmashauri ni kumuondoa Mkaguzi wa Ndani kuwa chini ya Mkurugenzi, hiyo
itaongeza uwajibikaji na ulinzi wa fedha," alisema Bw. Shemboza.
|
Posted: 04 May 2012 12:20 AM PDT
Mbunge
Mteule wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Bi, Shyrose
Bhanji, akisikiliza mada mbalimbali wakati wa maadhimisho ya Siku ya
Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, Dar es Salaam jana, kushoto ni
Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, (Viti Maalumu) Mkoa
wa Mara, Bi, Ester Bulaya. (Picha na Charles Lucas)
|
Posted: 04 May 2012 12:01 AM PDT
Na Florah Temba, Kilimanjaro
WANANCHI
mkoani Kilimanjaro wametakiwa kujijengea tabia ya kupima ardhi na
kuweka kumbukumbu kwa njia ya maandishi hatua ambayo itasaidia kuondoa
tatizo la migogoro ya ardhi baina ya wanandugu ambalo limekuwa
likiyakumba maeneo mengi mkoani humo.
Rai
hiyo ilitolewa na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Upimaji Ardhi na
Uendelezaji wa Makazi mkoani hapa Bw. Evans Ngolly wakati akizungumza na
waandishi wa habari ofisini kwake kuhusiana na changamoto
wanazokabiliana nazo katika suala la upimaji ardhi kwenye jamii.
Bw.
Ngolly alisema utaratibu wa upimaji ardhi katika familia nyingi mkoani
Kilimanjaro hauko bayana hali ambayo imekuwa ikisababisha kuzuka kwa
migogoro baina ya wanandugu.
Alisema, ni vema wananchi
wakajiwekea utaratibu wa kupima maeneo yao na kuweka bayana taarifa kwa
maandishi ili kuepuka matatizo ya migogoro ya mara kwa mara isiyo ya
lazima katika familia ambayo imekuwa ikichangia kurudisha nyuma jitihada
za kujiletea maendeleo.
“Upimaji ardhi kwa familia nyingi hauko
bayana, yaani ni kwamba wananchi wengi katika mkoa huu bado wamekuwa na
taratibu za upimaji ardhi (Vuhamba) kizamani hawaweki taarifa kwa njia
za maandishi na hali hii imesababisha kuwepo kwa migogoro baina ya
wanandugu pindi mmoja anapotaka kupima ardhi yake na kupewa hati miliki
ambapo kila mmoja huibuka na kusema sehemu hiyo ni yake,”alisema Bw.
Ngolly.
Bw. ANgolly alisema changamoto nyingine wanayokumbana
nayo ni pamoja na wananchi wengi kutokuwa na uelewa wa upimaji ardhi na
kupata hati miliki hali ambayo inawafanya wengi kuogopa kujitokeza
kupima ardhi zao.
Kutokana na hali hiyo Meneja huyo aliwashauri
wananchi mkoani Kilimanjaro kuona umuhimu wa kupima ardhi ili kuweza
kuepuka migogoro ya mara kwa mara ambayo inautesa mkoa huo katika maeneo
mengi.
|
Posted: 03 May 2012 11:59 PM PDT
Na Timothy Itembe, Mara
MBUNGE
Rorya mkoani Mara Bw. Lameck Airo amekabidhi mradi wa visima viwili kwa
nyakati tofauti uliogharimu sh. milioni 12 ndani ya kata za Rablwoo na
Kisumwa jimboni humo.
Akikabidhi visima hivyo jana kwa wananchi
Bw.Airo alisema kuwa amelazimika kuwachimbia wananchi wake visima kwa
kuwa ni moja ya ahadi aliyoahidi wakati wa kampeni zake.
Mbunge
huyo alisema, kwa hali hiyo hana budi kutimiza kutokana na ukame unao
ikumba wilaya hiyo wa mara kwa mara na kusababisha kuwepo uhaba wa maji.
Alisema,
maji hayo yatawasaidia akina mama na watoto wanaotumia mwendo mrefu
kwenda kuteka maji sehemu za mbali hususanimtoni na kwenye visima
visivyo salama. Aidha Bw. Lakairo alifafanua kuwa mradi huo
uligharimu sh. milioni 12 chini ya usimamizi wa Shirika lisilo la
Kiserikali, Global Resource Alliance.
"Watakao nufaika na mradi
huo ni Kata ya Rablwoo, Kijiji cha Buturi na Rablwoo pamoja na kitongoji
cha Kitongo na Nyamisingisi vya kijiji cha Kisumwa kata ya Kisumwa,"
alisema.
Mkurugenzi wa shirika hilo Bi. Ester Raphael alisema
kuwa shirika lake linajishugulisha na uchimbaji wa visima virefu na pia
linahudumia watoto waishio katika mazingira hatarishi.
Naye Mkuu
wa Wilaya ya Tarime Bw. John Henjewele ambaye alikuwa mgeni rasmi katika
hafla hiyo alisema kuwa ni wabunge wachache wenye moyo wakujituma kama
Bw. Lakairo kwa hali hiyo wananchi wamuunge mkono katika suala zima la
maendeleo.
Pia Bw. Henjewele aliongeza kuwa maji hayo yatumiwe
bila ubaguzi na ukoo na kamati hiyo ipange bei itakayokubalika ambayo
itasaidia kuendesha mradi huo katika matengenezo na mambo mengine
yatakayojitokeza.
Aidha, aliongeza kuwa kamati itakayochaguliwa
ishirikishe vijana wa shule zilizo karibu watatu kutoka shule za
sekondari na watatu kutoka shule za msingi.
|
No comments:
Post a Comment