N.I.H.F -KIKOA

N.I.H.F -KIKOA
N.I.H.F -KIKOA

FOREPLAN CLINIC

FOREPLAN CLINIC
FOREPLAN CLINIC

Saturday, May 5, 2012

UWT KIVUKONI WATANGAZA NAFASI ZA UONGOZI



UMOJA wa Wanawake nchini (UWT),  Kata ya Kivukoni wilaya ya Ilala umetangaza nafasi mbalimbali za uongozi kwa wanachama wake katika kata hiyo ambapo uchukuaji fomu umekwishaanza tangu Mei 4 mwaka huu.Katibu wa Umoja wa Vijana Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Kata hiyo, Omary Omary alisema hayo jijini Dar es Salaam leo, kuwa mwisho wa uchukuaji fomu hizo utakuwa Mei 11 mwaka huu.
Alisema nafasi zinazopaswa kugombaniwa na wanachama wa chama hicho ziko nane (8), ambapo kila mwanachama hai anayo nafasi ya kujitokeza katika kuomba moja ya nafasi hizo.
Omary alizitaja nafasi hizo kuwa ni pamoja na Mwenyekiti nafasi moja, Katibu nafasi moja, wajumbe wa kamati ya utekelezaji wanatakiwa wanne, Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Kata nafasi moja.
Nafasi nyingine ni wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Wilaya nafasi mbili , mjumbe wa Halmashauri ya Kata nafasi moja , mwakilishi kutoka UWT kwenda Wazazi nafasi moja na mwakilishi kutoka UWT kwenda Uvccm nafasi moja .
Omary alitanabaisha kuwa fomu zinapatikana katika ofisi ya CCM kata ya Kivuko kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 10:jioni ambapo kila fomu moja muombaji atapaswa kuilipia shil. 10,000/=.

No comments:

Post a Comment

Blog Archive